Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali (hawapo pichani) kujadili Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, hivi karibuni mjini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, wakijadili utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, hivi karibuni mjini Dodoma.
Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge, Mhandisi Leonard Masanja, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi huo, wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali (hawapo pichani), kilichofanyika hivi karibuni mjini Dodoma
Ramani ya Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge, utakavyoonekana baada ya kukamilika.
Wajumbe mbalimbali wakichangia hoja katika kikao cha Makatibu Wakuu, kilichojadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kutoka katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge.
Na Veronica Simba
Makatibu
Wakuu wa Wizara mbalimbali, hivi karibuni walifanya kikao kujadili
hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kutoka
katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji katika eneo la Stiegler’s Gorge.
Kikao
hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi
Mwinyimvua, kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Aidha, kikao hicho pia kilijadili majukumu ya kila Wizara husika katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi huo.Akifungua
kikao hicho, Dkt. Mwinyimvua alieleza kuwa mahitaji ya umeme nchini kwa
sasa ni makubwa kutokana na kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda hali
inayosababisha huduma ya umeme wa uhakika kuhitajika zaidi ya muda
mwingine wowote.
“Serikali
ya Awamu ya Tano inaelekeza nchi kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo
Mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, hatua za makusudi za kuongeza
uzalishaji wa umeme kwa ajili ya viwanda zinahitajika.”
Kamishna
wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, akielezea
umuhimu wa Mradi huo kwa Taifa alisema kuwa umeme wa uhakika unahitajika
ili pamoja na mambo mengine kukidhi mahitaji ya mkakati wa kusambaza
umeme vijijini ambao unaendelea nchini kote.
Awali,
akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mradi husika katika kikao hicho,
Msimamizi wake, Mhandisi Leonard Masanja alieleza kuwa, Desemba 19 mwaka
huu, Wizara ya Nishati ilitangaza zabuni ya kumpata Mkandarasi wa
Ujenzi wa Mradi huo ambao utekelezaji wake unakadiriwa kuanza mwishoni
mwa mwezi Februari 2018.
Alisema
kuwa, mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, Rais John Magufuli aliamua
kuanza utekelezaji wa ujenzi wa Mradi huo ambao ulibuniwa na Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere miaka ya 1970.
Mhandisi
Masanja aliongeza kuwa, timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati,
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Barabara Tanzania
(Tanroads), iliundwa ili kufanya maandalizi ya Mradi na baadaye
kusimamia ujenzi mara baada ya Mkandarasi kupatikana. “Timu hiyo
iliungana na timu ya wataalam kutoka Ethiopia katika utekelezaji wa
jukumu hilo.”
Makatibu
Wakuu walioshiriki au kuwakilishwa katika kikao hicho ni kutoka Ofisi
ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango,
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Wengine
ni kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na
Wizara ya Maliasili na Utalii
SHARE
No comments:
Post a Comment