Mwandishi
Wetu, TJNCDF
Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya
Kuambukiza Tanzania (TANCDA) linaeleza kuwa karibu kila mtu anakabiliwa na
tatizo la msongo wa mawazo.
Kinachosababisha hali hiyo, TANCDA inaeleza
kuwa ni hali ya jumla ya maisha. Mazingira na mifumo ya maisha ambayo jamii
inaishi yanachagiza binadamu kujikuta anapata msongo wa mawazo.
Katika maswali hayo ukiona miongoni
yanakuhusu, unapaswa kuchukua tahadhari ili tatizo la msongo wa mawazo
lisikusababishie madhara.
Siyo rahisi mtu kujua madhara anayopata kama
yanatokana na msongo wa mawazo yanayomkabili kwa sababu hiyo TANCDA inashauri
jamii kuchukua tahadhari.
Miongoni mwa maswali mtu anayoweza kujiuliza
ni: Je, hatuwi na wasiwasi kuwa watu wanachunguza ngua tunazovaa?
Je, hatushikwi na hofu pale tunapovuka
barabara kuwa tunaweza kugongwa na magari? Je, hatuwi na wasiwasi pale tunaposhindwa
kumaliza kazi zetu kwa wakati?
Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo mtu
anaweza kujiuliza. Jambo ambalo mtu anapaswa kulizingatia ni kuwa jambo lolote
linalomsababisha mtu kuwa na hofu, woga, taharuki, kukosa raha au kushindwa
kutekeleza majukumu mengine ni sehemu ya mambo yanayomsababishia msongo wa
mawazo.
Je, tunapojikuta katika hali hii tufanye
nini? TANCDA inashauri njia rahisi za kukabiliana na msongo wa mawazo ni
kufanya mazoezi mara kwa mara na kuwa makini na jambo moja kwa wakati mmoja.
Njia nyingine, TANCDA inaeleza ni kumueleza
mtu wako wa karibu na unayemuamini kuhusu tatizo lako ili akusaidie kwa
ushauri.
Hali nyingine ya kukabiliana na msongo wa
mawazo ni kucheka na kushiriki kwenye michezo, sherehe na burudani kama vile
harusi, ubatizo na mikusanyiko ya dini.
Mtu anapaswa kujifunza kukubali kuwa hawezi
kushindwa kila kitu na kutojitwika mambo mengi kuliko anavyoweza kufanya kwa
wakati.
Kuwa na muda wa utulivu kwa dakika kadhaa na
TANCDA inakushauri ni vyema ukachukua muda dakika chache kila siku kwa kuzima
simu hasa pale inapokufanya uwe na majukumu mengi.
Makala haya yameandaliwa na Chama cha
Waandishi Wanaopambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TJNCDF). Maoni,
ushauri au maswali tuma tjncdf@gmail.com
au S.L.P 13695, Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment