Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh.
Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Shedeli Mikole Mwenyekiti wa CCM kata ya
Vigwaza wakati akiwa katika ziara ya kikazi kukagua huduma za maendeleo
na miradi mbalimbali inayotekelezwa jimboni humo, Mh. Ridhiwan Kikwete
ametembelea kata na vijiji vya Visezi, Buyuni , kata ya Vigwaza. na
Magulumatari, Kisanga Kata ya Talawanda, Bago na Msinune kata ya
Kiwangwa.
Sehemu ya Bidhaa zinazotengenezwa
na vikundi vya Kimaendeleo. Kikundi cha Jipe Moyo ambacho ni moja kati
ya vikundi vilivyofaidika na fursa za Mitaji Katika Halmashauri na
Mfuko wa Jimbo ambao upo chini ya Mbunge wa Chalinze wakionyesha kazi
zinazotokana na Mikono yao mbele ya Mbunge.
Mmoja wa wananchi akizungumza mbele ya Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze .
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh.
Ridhiwani Kikwete akikagua Nguzo za umeme zipatazo 60 katika Kijiji cha
Visezi. ambazo zipo hapo toka mwaka 2015 sasa ni miaka miwili toka
Zilipoletwa hadi leo hazijaunganishwa. Serikali kupitia mradi wa
Peri-Urban Enlightment Initiative watakuja waunganishia wananchi wa
Visezi.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa Mh. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa jimbo la Chalinze.
SHARE
No comments:
Post a Comment