Maafisa wa kuzima
moto wameitwa katika jumba la Trump Tower katika kisiwa cha Manhattan
jijini New York kuzima moto uliokuwa umezuka kwenye ghorofa ya juu ya
jengo hilo.
Shirika la habari la CBS News limesema moto huo ulizuka mwendo wa saa moja asubuhi saa za huko (saa sita mchana GMT) karibu na paa la jumba hilo la ghorofa 68.
Trump alitumia jumba hilo kama makao na afisi yake kabla ya kuapishwa
Jumba hilo lilikuwa makazi rasmi ya Bw Trump kabla ya kuapishwa kwake karibu mwaka mmoja uliopita.
CBS News wamepakia picha za wazima moto wakiwa kwenye paa la jumba hilo huku moshi ukifuka kutoka kwa sehemu moja ya jumba hilo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment