Mkuu
wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kushoto)
,akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha
kitengo cha IT,wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya
la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es
Salaam .
Afisa
mauzo wa Airtel Juma Hassan (katikati) ,akifafanua jambo kwa baadhi ya
wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT,wakati
walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika
ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT wakiwa katika picha ya
pamoja na Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana
Lyamba (katikati) na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakati walipofanya
ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za
makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa chuo cha usimamizi wa fedha kitengo cha IT wakimsikiliza afisa
masoko wa Airtel Tanzania Prosper Mwanda ( kulia) wakati walipofanya
ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo na kuweza kutembelea
baadhi ya sehemu za katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es
Salaam.
-Wanafunzi wa IT wa chuo IFM wahimizwa kushirikiana na Airtel
WANACHUO kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) kitengo cha IT ,
wamefanya ziara ya mafunzo kwenye duka la kisasa la Airtel Expo
lililopo katika ofisi kuu za Airtel mtaa wa morroco Dar es salam ikiwa
ni mwendelezo wa kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora za kibunifu
kwa wateja wake.
Wanachuo hao waliweza kujifunza mambo mengi juu ya kampuni hiyo
inavyofanya kazi kuanzia huduma zake hadi bidhaa zinazouzwa na kampuni
hiyo. Ikiwemo Modem iliyozinduliwa hivi karibuni maarufu kama modem ya
maajabu Wingle Modem inayouweza kutumika na zaidi ya watu 10 kwa wakati
mmoja, Simu za Kisasa za gharama nafuu na zenye OFA nzuri
Wanafunzi hao pia wamejionea jinsi duka la Airtel Expo
linavyohudumia wateja wengi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya
kidigitali.
Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba
amewapongeza wanafunzi hao kwa dhamira yao ya kutaka kujifunza katika
ulimwengu wa technolojia na kuwakaribisha wengine kuhudhuria'
tumefarijika sana kuona wanafunzi toka vyuo vya ndani ya nchi yetu
kama nyie IFM mnafunga safari na kuja kushuhudia hili, hongereni sana
tunawakaribisha wote sio tu wanafunzi bali kila mpenda maendeleo ya
technolojia kutembelea duka hili la kisasa na kujionea au kushauriana na
Airtel kufanya mambo mengi bora zaidi ya ulimwengu wa mawasiliano"
alisema Bi Lyamba.
SHARE
No comments:
Post a Comment