Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu
ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo
wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana
maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Bao
la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili
lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu
likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kabla
ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana
Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa
kukabidhiwa bendera.
Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha na habari/ Faustine Ruta.
Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa KaitabaViongozi mbalimbali walikuwepo
Mgeni rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Serengeti Boys
Mgeni Rasmi na viongozi wengine wakisalimiana na Viongozi na wachezaji wa akiba wa Burundi
Nyimbo za mataifa yote mawili ziliimbwa kabla ya mechi kuanza
Taswira kabla ya mtanange
Viongozi wa Timu ya Serengeti Boys
Serengeti Boys wakipasha kabla ya Mtanange
Picha ya pamoja manahodha na waamuzi
Kipindi cha pili kilimalizika Serengeti Boys wakiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Timu ya Burundi. Picha na habari/ Faustine Ruta.Wanaangalia Mubashara bila Kiingilio!!!
Mchezaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola wa Serengeti akiendesha mpira kipindi cha pili
Oscar Mkomola(katikati) wa Timu ya Serengeti akiwekwa kati
Kim
na Bakary Shime wakiteta huku mtanange ukionekana kuwa mtelezo kwao
kipindi cha pili katika mchezo wa karafiki leo kwenye Uwanja wa Kaitaba
Mjini Bukoba. Kocha Bakar Shime ataiongoza tena Serengeti Boys siku ya
Jumamosi kwenye mchezo wa pili.
Kipa hakuona kitu!
Nahodha
wa Serengeti Boys Kevin Nashon Naftali dakika ya 72 ndiye
aliyewafungia bao hilo baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa
kuunawa mpira ndani ya boksi.
Mchezaji wa Serengeti Boys (kushoto) akipeta kwa bao lao la tatu
Bao tatu 3-0
Serengeti wakifurahia moja ya bao la mkwaju wa penati
Shangwe! 3-0
Chupuchupu afunge bao lingine!
Clement Kibabane akimiliki mpira kipindi cha pili mwishoni
Kibabane tena na mpira
Mchezaji wa Serengeti Boys (kulia) Ibrahim Abdallah Ally akimnyatia mchezaji wa Burundi
Burundi wakiwa hoi baada ya kuzidiwa ujanja
Dakika 90 zilikamilika hivi....
SHARE
No comments:
Post a Comment