
Mbunge wa
Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi jezi seti 20 na mipira 20
kwa walimu na manahodha wa shule zote za Sekondari zilizopo wilayani
humo jana .shule hizo hivi sasa zipo kwenye maandalizi ya mashindano ya
UMISETA Picha na David John
MBUNGE wa
Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi jezi seti20 na mipira 20
zenye thamani ya sh.milioni 4katika shule zote za Sekondari zilizopo
katika Jimboni hapa.
Akikabidhi
jezi hizo wilayani hapa jana katika hafla fupi iliyowakutanisha walimu
wakuu,wanamichezo,watendaji wa halmashauri ,pamoja na Ofisa Elimu ,Ulega
amesema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika
juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
Amesema
kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku
akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
“Ndugu
zangu walimu na manahodha wa timu zote Kutoka shule 20 za sekondari
zilizoponda ndani ya Jumbo langu la Mkuranga nimetoa vifaa hivi ili
muweze kushiriki vyema katika michezo ya shule za Sekondari UMISETA
nakutuletea mafanikio,”alisem Ulega
pia
amesema kuwa anatambua kuwa kuna changamoto za kutosha katika michezo
hususani vifaa vya michezo Kwa kutambua hilo ameamua kutoa vifaa hivyo
huku akiwataka wanafunzi na walimu hao kusimamia vyema.
Aidha
Mbunge Ulega amehaidi kutoa ushirikiano wa dhati Kwa walimu na viongozi
mbalimbali wa halmashauri hiyo ili Kwa pamoja kuharakisha maendeleo
jimboni hapa ikiwamo michezo.
Pia
amewaambia viongozi hao kujenga mashirikiano ya Katibu na yeye kama
mwakilishi wao yupo tayari Kwa wakati wowote kutumika na kusikiliza
maoni yao.
Kwaupande
wake Ofisa Elimu wa Halmashauri Kwa upande wa shule za Sekondari
Benjamini Majoya akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa Mbunge Ulega
amefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa Kwa viongozi wengine
waliotangulia.
Amesema kuwa watamuunga mkono Mbunge huyo Kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika nyanja ya Elimu na michezo Kwa ujumla.
“Kwanza
tunashukuru Kwa vifaa hivi kwani vimekuja katika wakati muhimu ambapo
tunakwenda katika mashindano ya UMISETA na Kwa vifaa hivi ushindi
upo,”amesema Majoya
Pia
ameongeza kuwa hakuna ubishi kwamba michezo ni ajira hivyo lazima
watahakikisha vijana hao wanafanya vizuri katika michezo na taaluma pia(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment