
Watu 60,000 wamekusanyika katika mji wa Brussels wakipinga dhidi ya marekebisho ya sheria ya kazi Ubelgiji.
Na RFI
Wafanya
fujo, waliofukuzwa na polisi kwa kutumia mizinga ya maji, wamevuruga
maandamano makubwa mapya yaliyokua yamefikia ukingoni nchini Ubelgiji
dhidi ya mageuzi, hasa ya sheria ya kazi, yanayopangwa kufanywa na
serikali ya mrengo wa kulia.
Maandamano
ya watu wapatao 60,000, kwa mujibu wa polisi, yamevunjwa karibu na eneo
la Gare du Midi mjini Brussels ambapo mamia ya wafanya fujo, baadhi
wakiwa wamejificha nyuso zao kwa fulana au vifaa vya kujilinda na gesi,
walianza kutupa vilipuzi dhidi ya polisi, ambayo ilijibu kwa mizinga ya
maji.
Waandamanaji
wanane na askari polisi wawili, ikiwa ni pamoja afisa mmoja,
wamejeruhiwa, kwa mujibu wa polisi, iliyonukuliwa na shirika la habri la
Belga.
Maandamano,
ambayo yaliitishwa na vyama vya vikuu vya wafanyakazi nchini Ubelgiji
lakini pia chama cha Kisoshalisti (PS) ambacho kiko katika kambi ya
upinzani tangu uchaguzi wa mwaka 2014, tangu wakati huo yalikua
yakiendeshwa kwa utulivu, waandamanaji wakizunguka maeneo makuu ya
katikati ya mji mkuu wa Ubelgiji katika hali ya utulivu na amani.
Katika
msafara wa maandamano hayo, waandamanaji kutoka mikoa ya Flanders
(kaskazini), Wallonia (kusini) na Brussels walikua wamebeba mabango
ambayo yalikua yameandikwa kama vile "hapana kwa wiki ya masaa 45",
"isiguswi pensheni yetu" au pia "Hapana mabadiliko "na walikuwa
wakilipua maputo mengi.
Mwaka
mmoja na nusu baada ya kuingia madarakani muungano wa mrengo wa kulia wa
Waziri Mkuu Charles Michel, uhamasishaji wa vyama vya wafanyakazi na
vyama vya kisiasa vya mrengo wa kushoto kumeendelea kuwa na nguvu.
Migomo kadhaa ilishuhudiwa mwaka 2014 baada ya maandamano makubwa katika
mji wa Brusselsmwezi Novemba 2014, ambapo watu 120,000 walishiriki,
kamwe tukio hilo lilikua halijaonekana kwa miongo kadhaa nchini
Ubelgiji. RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment