![]() |
Wananchi na maofisa wa polisi wakitazama ajali ya gari aina ya RAV4 iliyoua ndugu watatu akiwemo mke na mme waliokuwa wakienda Mbinga Ruvuma katika mazishi leo huku watatu wakijeruhiwa |
![]() |
Hii ndio ajali iliyoua watatu leo Iringa |
![]() |
Na Matukio Daima Blog |
WATU watatu ambao walikuwa wakielekea
mkoani Ruvuma katika msiba
akiwemo mke na mume pamoja na mfanyakazi wa ndani wamefariki dunia
papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya gari ndogo
waliokuwa wakisafiria kwenda msibani kugongana uso kwa uso na lenye
namba za usajili T 866 DMC Mitsubishi Canter.
Imeelezwa kuwa wanafamilia hao waliokuwa wakisafiri katika gari aina
ya RAV 4 yenye namba za usajili T 795 DGD walikuwa wakielekea
Mbinga mkoani Ruvuma kwa ajili ya kushiriki shughuli za mazishi walipata
ajali hiyo eneo la Kisolanza katika wilaya ya Iringa kwenye
barabara kuu ya Dar es Salaam - Ruvuma .
Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaimaeneo la tukio ndugu wa karibu
na marehemu hao Negro Sanga alisema kuwa alipigiwa simu majira ya saa 12
asubuhi ya leo na ndugu waliopo Dar es Salaam wakimtaka kufika eneo
la tukio ili kutoa msaada kwa majeruhi hao ambao walikuwa
wamepata waliwapigia simu kuomba msaada .
" Hawa ndugu zangu walikuwa wakielekea Mbinga mkoani Ruvuma kwa ajili
ya kushiriki mazishi na nimeshitushwa sana baada ya kupigiwa simu ya
rafiki yangu kutoka Dar es Salaam asubuhi sana kuniomba nifuatilie
ajali hiyo kwani walikuwa hawana msaada kwa asubuhi hiyo ndipo
nilipojulisha polisi ambao walifika kwa wakati eneo la tukio na
kusaidia kuokoa maisha ya majeruhi watatu "
Sanga alisema kuwa baada ya kufika eneo hilo la ajali tayari
wasamaria wema walikuwa wameitoa miili mitatu ya marehemu hao huku
majeruhi wakiwa wametolewa kutoka katika gari hilo ambalo baada ya
kugongana na lori hilo liligeuka kuelekea mwelekeo ambao lilikuwa
likitoka huku Lori likiwa limepinduka upande wa pili wa barabara .
“ Waliopoteza maisha katika ajali hii ni mume ambae alikuwa ndie dereva
,mke wake aliyekuwa amekaa siti ya mbele pamoja na kijana wao wa kazi
aliyekuwa siti ya nyuma kwa dereva pamoja na watu wengine watatu ambao
walijeruhiwa vibaya “
Hata hivyo Sanga anasema katika ajali hiyo inaonyesha mmoja
wapo alikuwa
amesinzia na ndio sababu ya kugongana uso kwa uso huku akidai
kuwa majeruhi
wote wamekimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi kwa matibabu .
Dereva wa lori ambalo liligongana na gari ndogo hiyo Issa Markus
alisema kuwa
eneo hilo ni eneo ambalo lina mteremko kiasi na wakati akimaliza kushuka
mteremko huo gafla dereva wa gari ndogo hiyo iliyokuwa ikitokea
mbele yake
alihama upande wake na kuja upande wake na alipojaribu kumkwepa kwa
alirudi upande wake kabla ya kumfuata tena na ndipo walipoishia
kugongana .
“ Inaonyesha dereva mwenzangu ambae sasa ni marehemu alikuwa amesinzia
maana nimefanya jitihada kubwa sana za kumkwepa ila bado kanifuata kama
unavyoona lori langu likiwa limepinduka hii yote ni katika jitihada za
kumkwepa …..mimi na utingo wangu tumetoka salama ila mimi
nimejeruhiwa kidogo
sikio la kulia”

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi ameuthibitishia mtandao wa matukiodaimablog kutokeakwa ajali hiyo na kuwa ilitokea majira ya saa 10 alfajiri na
kuwataja walipoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Anord Conrad Kapinda (46) mkazi wa
Kigamboni mkoani Dar es Salaam ,Maimuna Gwangaya (45) na Joshua Aidan
ambae ni fundi selemara Mbagala jijini Dar es Salaam.
Alisema majeruhi wa ajali hiyo ni Neema kapinga (26 ) mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Dar es Salaam , Yohana Fortino ( 22) Fortino Kapinga (55) wamekimbizwa
Hospitali ya wilaya ya Mufindi kwa matibabu huku akiwataka madereva kuacha kulazimisha
safari majira ya usiku na pale ambapo wanahisi kuwa na usingizi ni
vema kuegesha gari na kupumzika .

SHARE
No comments:
Post a Comment