Meneja wa
kituo cha huduma kwa Wateja Bw.Juma Msabaha akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja
kilichozinduliwa hii leo Makao makuu ya Benki hiyo,Golden Jubilee towers
Daresalam. Sasa wateja na wasiokuwa wateja wa benki hiyo wataweza
kupata maelezo kuhusiana na mikataba ya mikopo inayofuata mifumo ya
kiislamu, kutoa msaada katika matumizi ya huduma zetu mbadala kama ATM,
Internet Banking, Amana Bank Mtaani, Amana Mobile na huduma nyingine
mbalimbali.
Sehemu ya
waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo wakisikiliza kwa makini
uzinduzi wa kituo hicho. Imeelezwa kuwa kituo hicho kitasaidia kusogeza
huduma karibu na wananchi na kutatua baadhi ya kero ambazo wateja
walikuwa wanakutana nazo.
Mkuu wa biashara wa AMANA BENKI Bw. Munir Rajab akifafanua jambo kuhusu kituo hicho.
NA SELEMANI MAGALI- DARESLAAM
BENKI ya
Kiislamu ya Amana imezindua kituo chake kipya cha huduma kwa wateja kwa
njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuboresha
huduma kupitia teknolojia ya mawasiliano
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Meneja Mwandamizi Huduma
kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Juma Msabaha alisema uzinduzi wa kituo
hicho umelenga kuboresha mahusiano ya wateja pamoja na kusogeza huduma
za kibenki karibu na wananchi.
Akifafanua
kuhusu kituo hicho, Bw. Msabaha alisema kituo hicho kitafanya kazi kwa
masaa 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku ambapo wateja wa
Amana na ambao bado hajabahatika kutumia huduma za benki hiyo watapata
fursa ya kuuliza masuala mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Benki.
“Tumejipanga vizuri, tunayo timu nzuri yenye uzoefu na masuala ya Kibenki ,watafafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma za Amana benki kuanzia masuala ya akaunti,miamala ya kimtandao na huduma zinazotolewa na mawakala wetu kote nchini.Alisema Msabaha.
Ameongeza kusema Kituo hicho kitafanya kazi siku saba katika wiki,pamoja na siku za siku kuu jambo ambalo wanaamini litasaidia kufafanua mambo mbalimbali yanayowahusu wateja.
“Namba yetu ya huduma kwa mteja ni 0657 980 000, kupitia namba hiyo ni matarajio yetu kuwa wateja watafurahia zaidi huduma tuliyoizindua kwani ni rafiki kwa kila mmoja, imeandaliwa mahususi kabisa kuwapa uwezo wananchi kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi pamoja na njia zingine za mitandao ya kijamii”.Alisema Msabaha
Kwa mujibu wa Bw Msabaha kituo hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye biashara kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa bora na ni hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia kuwa na matokeo mazuri
Alibainisha kuwa huduma hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha pamoja na hadhi yao hatua aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo uaminifu miongoni mwa wateja wake
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Biashara ya Amana Benki Bw. Rajab Munir amesema wateja wa Amana watapata fursa ya kuijua benki yao kwa undani kwani sasa wanaweza kuulizwa maswali yao na kujibiwa kwa wakati ndani ya masaa 15 katika wiki ikiwamo siku za siku kuu.
Alisema hiyo ilikuwa dhamira yao ya muda mrefu na kuzinduliwa kwake imekuwa ni faraja kwa wateja ambao sasa watafaidika nayo.kwa kupata majibu ya papo kwa hapo kuhusiana na akaunti zao, miamala yao na misaada kuhusu kutumia huduma za kimtandao.
katika kipindi kisichopungua miaka mitano Tayari Benki ya Amana kwa imefanikiwa kuwa na matawi saba matano yakiwa katika Jiji la Daresalaam na mengine mawili yakiwa katika Jiji la Mwanza na Arusha.
Mipango ya Baadae ni kwamba Amana benki inatarajia kufungua matawi mengine si chini ya matatu kati ya Mkoa wa Tanga au Zanzibara kulingana na upembuzi yakinifu utakaofanywa na benki hiyo. (P.T)

SHARE
No comments:
Post a Comment