Waziri wa
Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama
akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa
Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji
uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Wadau
kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa
makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu
Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa
Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika jana
jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa
kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuwa mdhamini wa Mkutano
wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Mkurugenzi
Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto wakati wa ufunguzi
wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Waziri Mkuu Dkt.Hamis Mwinyimvua wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa
Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika jana
jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali
imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili
kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.
Akizungumza
kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa
Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama
amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana
katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwakwamua vijana katika
uchumi.
“Tunatambua
vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua
uchumi wan chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila
bajeti tutatenga bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi.
Mhagama.
Aidha
Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya
sheria itakayowawezesha wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi wa
nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya
Bima (ARIS) Bw. Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali
imeweka mkakati wa kupitia upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu
wafanya biashara kumiliki uchumi kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi
hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa uchumi wa nchi.
Naye
Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema
kuwa ipo haja ya watanzania hususani wakulima washirikishwe kwenye
semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia 60 ya
watanzania ni wakulima.
Mkutano
huo wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji
umeandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi(NEEC)
kwa lengo la kujadili jinsi ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua
kiuchumi limeanza Julai 21 na kumalizika 22 Julai mwaka huu. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment