Mwashamu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara akikata keki wakati wa sherehe za
kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania jana Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, katikati ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendejana.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam yaliyoanza rasmi tangu
April 26 mwaka huu. Katikati ni Mwashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki
la Mtwara Titus Mdoe,kutoka kulia ni Mhamasishaji Mkuu wa Redio Maria
Tanzania Bi. Veronica Mwita na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendejana.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Baba Askofu wa Jimbo
Katoliki la Mtwara Mwashamu Askofu Titus Mdoe wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es
Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre. John
Maendejana.
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Saalam Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo akizungumza na wadau na marafiki wa Redio Maria Tanzania jana
Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea
kuanzishwa kwa Redio hiyo
Mkurugenzi
wa Redio Maria Tanzania Padre John Maendeleo akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Rais wa
Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipokea risala kutoka kwa Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius
Kira(Kulia) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipeana mkono na baadhi ya marafiki wa Redio Maria Tanzania waliofika
kuchangia Redio hiyo katika harambee iliyofanyika ikiambatana na sherehe
za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania jana Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Rais wa Redio Maria Tanzania Bw. Humphrey Julius
Kira.
Baadhi ya waumini wa Roman Katoliki wakifurahi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania (RMTZ). Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Rais
wa Redio Maria Tanzania, Humphrey Kira ameiomba Serikali kurekebisha
Sheria ya leseni ya redio za jamii ili ziweze kuwa na vituo vingi vya
kurushia matangazo yake.
Hayo
yamesemwa jana na Rais huyo wakati alipokuwa akisoma risala kwenye
sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya redio hiyo
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre, Jijini Dar es Salaam.
Kira
amefafanua kuwa redio za kijamii hasa zilizojikita katika nyanja za
kiimani zinasaidia kufundisha maadili na kufanya wananchi wakomae
kiimani, hivyo angefurahi sana kuona redio za aina hiyo zinapewa leseni
za kurusha matangazo yake nchi nzima.
“Ndugu
mgeni rasmi, redio yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na ufinyu wa sehemu za usikivu (coverage areas) ambapo tatizo
hili linatokana na sheria ya leseni za redio ambayo hairuhusu redio za
aina hiyo kuwa na vituo zaidi ya kumi nchini nzima, tunaomba serikali
itusaidie kuiboresha sheria hii ili tuongeze vituo vya matangazo ya
dini”, alisema Kira.
Rais
huyo ameongeza kuwa majimbo yote yanahitaji kufikiwa na huduma za
maombi, hivyo anawashauri wasikilizaji wote kuendelea kuisikiliza redio
hiyo kwa njia ya mitandao ikiwemo simu za mkononi kwani hivi sasa huduma
hiyo inapatika nchi nzima.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa rai kwa uongozi wa redio hiyo
kutobadilisha maudhui wala kuweka vipindi visivyokuwa vya dini ili
iendelee kuunganisha familia na sio kuzigawa familia.
“Tunasema
kuwa redio Maria ni sauti ya kikristu nyumbani mwako lakini mimi nasema
ni sauti ya Mungu ndani ya familia kwa kuwa inafanya kazi ya
kuunganisha familia, vyombo vingine vya habari vinafanya kazi kubwa ya
kuigawa familia lakini Redio Maria ni tofauti”, alisema Pengo.
Askofu
Pengo amewashukuru wananchi wote waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo
kwa kuwa kufanya hivyo ni njia moja wapo ya kumuenzi na kumpa heshima
Mama Bikira Maria.
Nchini
Tanzania, Redio Maria ilianzishwa Aprili 26 mwaka 1996 katika Jimbo Kuu
Katoliki la Songea ikiwa na lengo la kumsaidia Mama Bikira Maria katika
kazi yake ya kumtangaza Yesu Kristo kwa watu wote. Mpaka sasa ina vituo
10 Tanzania Bara na viwili Zanzibar. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment