Na Beatrice Lyimo-MAELEZO Dar es Salaam
SERIKALI
imesema sekta ya kilimo inaendelea kuwa sekta muhimu katika uchumi wa
Tanzania kwa asilimia 25% ya pato la taifa na kuajiri asilimia 75% ya
watanzania wakiwemo wanawake na vijana.
Hayo
yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Richard Kasuga wakati wa uzinduzi wa
mchezo wa redio uitwao KUMEKUCHA unaotarajia kuonyesha mchango wa
wanawake na vijana katika kutokomeza tatizo la uhaba wa chakula nchini.
Kasuga
amesema kuwa igizo hilo la mchezo wa redio, litaakisi umuhimu wa
ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kukuza sekta ya kilimo na
kutoa ujumbe kwa vijana kuona umuhimu wa kilimo hasa kilimo cha
biashara.
“Sheria
na tamaduni zilizopo zinakwaza juhudi za mwanamke kupata fursa za
kiuchumi kwa sababu hawana haki ya kumiliki ardhi au vifaa vya kilimo,
vyanzo endelevu vya maji, ukosefu wa mikopo ambayo wanahitaji ili
kufanikisha juhudi zao”alisema Kasuga.
Kwa
upande wake mwakilishi kutoka shirika la msaada la Marekani (USAID)
Randy Chester alisema kuwa mchezo wa KUMEKUCHA umeandaliwa na taasisi ya
Africa Lead kwa kushirikiana na Media for Development International
(MFDI) na kufadhiliwa na USAID kwa lengo la kupunguza uhaba wa vyakula
vyenye virutubisho hapa Tanzania.
Mchezo wa
KUMEKUCHA ni mchezo wa redio wa kila wiki ambao unaangazia maisha,
vikwazo na fursa za wakulima Tanzania na utaanza kurushwa hewani kuanzia
Julai 25, 2016 kupitia Redio Free Afrika, Redio Abood FM, Redio Ebony
FM na Redio Bomba FM. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment