Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla ametoa maagizo mazito kwa watendaji wa Wizara hiyo
kesho tarehe 22 Agosti.2016 kuhakikisha wanamfikishia taarifa ya kina
kuhusu upungufu wa chanjo nchini.
Akiwa
ziara ya kikazi Mkoani Geita, Ameagiza akute maelezo ya kina mezani
kwake, kuwa ni nani haswa amesababisha chanjo kupungua kwenye maeneo
mengi nchini? Na mpaka sasa amechukuwa hatua gani za kuwajibika?
Je, changamoto ipo hazina ama kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za
kinga? “Vyovyote vile, nataka utetezi uje ukiwa na vielelezo, kabla
sijachukua hatua stahiki. Chanjo ni eneo pekee kwenye sekta ya Afya
tulilofanikiwa kwa zaidi ya 95%! Haikubaliki kurudisha nyuma mafanikio
haya."
Alisema, Baadhi ya maeneo chanjo zipo na wana dozi za mwisho na baadhi hazipo kabisa. Mfano
bohari ya chanjo Mkoa wa Geita hakuna chanjo za OPV, Rotavirus, BCG na
Tetanus. Wangepaswa kuwa na akiba ya miezi mitatu mbele. Kwenye ngazi ya Taifa wanapaswa kuwa Na chanjo za miezi Sita mbele, hapo ndipo tunaweza kusema tuna chanjo za kutosha.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dk. Brayan Mawalla na Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Geita Dk. Joseph Kisala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua
sehemu ya dawa kwenye duka la Hospitali hiyo ya Mkoa wa Geita
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk.
Joseph Kisala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla katika ziara
hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (hayupo pichani)
Mbunge wa Geita Mjini Mh. Constantine John Kinyasu akitoa maelezo kwa watendaji wa hospitali ya Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa
maelezo kwenye bohari ya dawa za chanjo ya mkoa wa Geita
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa maagizo kwa
watendaji wa Wizara yake kuhakikisha wanampelekea maelezo ya kina juu
ya upungufu wa chanjo hapa nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment