Polisi nchini
Argentina walimpiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati
kwenda gereza moja, kwa mujibu wa mamlaka za gereza.
Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na vidonge vya madawa ya kulevya.
Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa na ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi.
- Ndege za Pakistan zatumiwa kusafirisha heroin hadi Uingereza
- Mihadarati ya Cocaine ya pauni milioni 50, yapatikana Uingereza
- Baba mkwe wa El Chapo Guzman afungwa miaka 10
Magereza nchini Argentina yalionya mwaka 2013 kuwa walanguzi wa madawa ya kulevya walikuwa wakitumia njiwa waliokuwa wakifanya safari mara 10 hadi 15 kwa siku.
Watu watatu walikamatwa na njiwa 15 kupatwa baada ya uchunguzi wa mwaka 2013.
Mapema mwaka huu njiwa ambaye alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya alishikwa nchini Kuwait karibu na mpaka na Iraq.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment