Na Abushehe Nondo (MAELEZO).
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Bw.Godwin Gondwe amepiga marufuku wananchi wa
wilaya yake kucheza mchezo wa bao na “pool table” wakati wa mchana muda
ambao ni wa kufanya kazi ili kutekeleza falsafa ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya “Hapa kazi Tu”.
Gondwe
alitoa kauli hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati
akizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu wilaya yake ya Handeni ambapo
alisema katika wilaya hiyo baadhi ya vijana hawana muamko wa kufanya
kazi badala yake wamekua wakijishughulisha na kucheza bao na “pool
table” vitu ambavyo haviwaletei maendeleo.
“Nimekataza
vijana katika wilaya yangu kucheza michezo ya bao na “pool table”
wakati wa kazi na nimewahamasisha kushiriki shughuli za ufugaji na
kilimo kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kuondokana na hali ya
umasikini” alisema Gondwe.
Mkuu
huyo wa Wilaya aliwashauri wakazi wa Handeni kujishughulisha na kilimo
cha mazao mbalimbali ya biashara ikiwemo alizeti, ufuta na ufugaji wa
mbuzi na kuku ili waweze kujipatia fedha zitakazowasaidia kujikimu
kimaisha.
Pia
Gondwe alisema kuwa wamekubaliana na Idara ya Ardhi wilayani humo
kutenga maeneo maalum ya uwekezaji kwa vijana ambapo Serikali
itawawezesha kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kilimo.
Amewataka
vijana kujiunga katika vikundi waweze kupatiwa fedha ambazo kila
Halmashauri imetenga kwa ajili ya vijana na wanawake na watumie mikopo
hiyo kujikwamua kimaisha kwa kufanya shughuli za ujasiliamali.
Akizungumzia
tatizo la ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo,
Gondwe alisema bado anaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali
kuhakikisha tatizo la maji wilayani Handeni linapungua ili wananchi
waweze kuondokana na adha hiyo ambayo inawakabili kwa muda mrefu.
Alisema
wananchi wa Handeni hasa wanawake wanapata tabu ya kutafuta maji safi
na salama ingawa Serikali bado inaendelea kushirikiana na wadau wa
maendeleo kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo kwa uhakika. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment