Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho 23 ya Sikukuu ya Wakulima Nane
Nane kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Sehemu
ya Wakazi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi
kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane ambayo
kitaifa yanafanyika mkoani Lindi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Luteni Joseph Benedict Lyakurwa wa Suma JKT alipotembelea
eneo lao na kujionea shughuli mbali mbali za kilimo na ufugaji kwenye
kilele cha maadhimisho ya 23 ya sikukuu ya wakulima ya Nanenane mkoani
Lindi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Daraja la kwanza Halima Kikwega
wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane , Ngongo Lindi.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwapungia wananchi mikono wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya
maonyesho ya Wakulima Nane nane mkoani Lindi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya
dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo kwenye kilele cha
maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane kitaifa katika uwanja wa
Ngongo Manispaa ya Lindi mkoani Lindi kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika
hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya
Ngongo, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi
maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali
katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii,
kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2020.
“Napenda
kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na
kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa
ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama
vyenu.”
Kuhusu
uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan amesema maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane ni moja katika
ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa
ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za
kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.
Amesisitiza
kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na
uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa
kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa
ujumla.
Makamu
wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango
inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa
kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi
16,478 kwa mwaka wa fedha m2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe
la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.
Aidha
amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo
kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na
serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi,
Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora
za mazao ya chakula nchini.
Kwa
Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amehimiza
wananchi kote nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana
zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze
uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi
katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.
SHARE
No comments:
Post a Comment