Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na wakazi wa
Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la
uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya
maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo kwa wakazi
wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi
la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya
maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
Baadhi
ya wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III katika kijiji
cha Mwamgoba Wilayani Busega, wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na katibu tawala Jumanne Sagini (hawapo pichani),
walipozungumza nao kabla ya zoezi la uhawilishaji wa fedha za ruzuku kwa
ajili ya mpango huo.
Bw.
Methesela Mrobi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine
wa Mkoa na Wilaya(hawapo pichani) Bwawa dogo alilochimba kwa kutumia
fedha za ruzuku za Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III, ambalo
analitumia kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji
Mkuu
wa Wilaya ya Busega , Mhe. Tano Mwera (katikati) na Katibu Tawala
Wilaya ya Busega, Bw. Sebastian Masanja (kulia) wakizungumza jambo kabla
ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa
kunusuru kaya maskini TASAF III kijiji cha Mwamgoba, Wilayani Busega
(kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akimkabidhi fedha Bw. Methesela
Mrobi wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa
Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III ,katika kijiji cha Mwamgoba,
Wilaya ya Busega Mkoani humo.
Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkoa wa Simiyu)
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na
vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III(PSSN)
wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa
mpango huo.
Mtaka
ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha
Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III
PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82
kijijini hapo.
Mtaka
amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali
ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa
ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule
lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala
ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo
pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.
“Hatuwezi kuleta fedha tukifikiri
zitawasaidia kujikwamua katika Umaskini lakini mnashinda baa na
vilabuni kulewa , wengine mnaongeza wake, tukiwabaini mtaondolewa kwenye
huu mpango” , alisema Mtaka.
Mtaka amewataka wanufaika hao kujishugulisha na kilimo na ufugaji na kuondokana na dhana ya kuwa watakuwa wanufaika wa mpango huo siku zote, ambapo alieleza azma ya Serikali
ya awamu ya tano ya kuwatoa wananchi katika umaskini na kuwaondolea
changamoto mbalimbali kama kutoa elimu ya bila malipo na kuanzisha Mfuko
wa Huduma ya Afya Watanzania wasio na uwezo waweze kupata matibabu kwa
gharama nafuu na
akatoa wito kwa wanufaika hao kujiunga na Mfuko wa Huduma ya Afya ya
Jamii (CHF)ambao utawasaidia wao wenyewe pamoja na wategemezi wao kupata
huduma za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.
Aidha,
ametoa wito kwa wazazi kuwakumbusha watoto wao wajibu wa kuwatunza kwa
sababu kumekuwa na baadhi ya wazee ambao wametambuliwa kuwa ni maskini,
wakati wana watoto wenye nguvu na uwezo wa kuwasaidia lakini hawatimizi
wajibu wao kuwatunza kwa kuwapa mahitaji muhimu.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa fedha hizo Bibi. Christina Robert ambaye ni
mnufaika wa mpango wa TASAF amesema mpango huo umemsaidia kuondokana na
kuishi katika nyumba ya nyasi na matope na kumuwezesha kujenga nyumba ya
matofali na bati.
“Naishukuru
TASAF maana imenisaidia sana, ruzuku niliyopewa mara ya kwanza
ilinisaidia kutibiwa nilipofanyiwa upasuaji, mara ya pili nilitumia tena
kwenye matibabu, mara ya tatu nilinunua kuku na bata, mara ya nne nikanunua bati nikajenga nyumba ya vyumba viwili”, alisema Christina.
Pamoja
na kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya fedha za ruzuku za TASAF Mtaka
amewataka wananchi wa Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuongeza
juhudi katika kilimo cha mazao ya mikunde kwa kuwa tayari Serikali ya
India imekubali kununua zaidi ya tani milioni sita ya choroko, dengu na
mbaazi kutoka Tanzania, hivyo
wakati utekelezaji wa makubaliano hayo utakapoanza wananchi walime kwa
wingi mazao hayo kwa kuwa kutakuwa na soko la uhakika.
Jumla
ya kaya 4260 zilibainishwa katika vijiji 41 vya wilaya ya Busega ambapo
kaya 53 ziliondolewa katika mpango wa TASAF III PSSN baada ya uhakiki
na kubaini kuwa hazikukidhi vigezo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment