Mmoja
wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Awali na Msingi
ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, akimuonesha mgeni rasmi wa
mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha
Mapunda (wa pili kushoto) darubini na jinsi inavyofanya kazi. Wanafunzi
65 wa shule hiyo wanatarajiwa kuihtimu elimu ya msingi mwaka huu.
Mwanafunzi
Bora katika somo la Sayansi katika Shule ya Awali na Msingi ya Genius
Kings ya jijini Dar es Salaam, Neema Richard akimuonesha mgeni rasmi
Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda(kulia), jinsi ya
kuhifadhi kiumbe mfu kwa kutumia ‘Formalin’.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Shule Dkt. Jesse James.Kushoto ni Mkurugenzi Julius Rutabanja
na Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Machage Kisyeri na wa tatu kulia
ni Mratibu wa Elimu Kata ya Segerea, Flora Vincent.
Wahitimu
wa darasa la saba katika Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya
jijini Dar es Salaam, Neema Richard na mwenzake wakimuonesha mgeni rasmi
Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda, chura aliyehifhadhiwa
kwa kutumia ‘Formalin’ katika maabara ya shule hiyo.
Mgeni
rasmi wa mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya
jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda,
akiangalia kifaa kinachotumika katika mfumo wa umeme wa kompyuta wakati
akitembelea maonesha ya wahitimu wa shule hiyo.
Mkurigenzi
Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es
Salaam, Machage Kisyeri akiingiza kijiti kilichowashwa moto ndani ya
‘test tube’ kuzalisha hewa ya oksijeni ikiwa ni sehemu ya maonesho ya
wahitimu wa shule hiyo wakionesha jinsi ya.Kulia ni mgeni rasmi wa
mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha
Mapunda, akishuhudia.
Kikundi
cha Skauti cha Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar
es Salaam, kipiga saluti wakati wa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza
kwa mahafali ya tano ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Kikundi
cha kwaya cha Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es
Salaam, wakiimba wimbo kwenye mahafali ya tano ya wahitimu wa darasa la
saba wa shule hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kikundi
cha Skauti cha Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar
es Salaam,kikionesha umahiri katika mchezo wa Karate kwenye mahafali ya
tano ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo yaliyofanyika jijini
Dar es Salaam.
Mkuu
wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam,
Aloyce Siyame akisoma ripoti ya shule kwa mgeni rasmi wa mahafali ya
tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha
Mapunda(hayupo pichani).
Mkuu
wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam,
Aloyce Siyame akisalimiana na mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya shule
hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda, kabla ya
kumkabidhi ripoti ya shule hiyo.
Mwanasarakasi akionesha ujuzi wake kwenye mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam.
Mkurungenzi
Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es
Salaam, Machage Kisyeri akiwasilisha Taarifa ya maendeleo ya shule hiyo
kwa mgeni rasmi.
Mkurungenzi
Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es
Salaam, Machage Kisyeri, akijumuika na wanafunzi wa shule hiyo kucheza
ngoma ya asili ya mkoani Mara.
Wahitimu
wa darasa la saba mwaka 2016 wa wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius
Kings ya jijini Dar es Salaam, wakiimba wimbo wa kuaga.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius
Kings ya jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha
Mapunda akizungumza katika hafla hiyo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Shule Dkt. Jesse James na kulia ni Mkurugenzi Mtengaji wa shule hiyo
Machage Kisyeri.
Mkurugenzi
wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam,
Imelda Machage (kushoto) na Mkurugenzi mwenzake Julius Rutabanja,
wakimkabidhi zawadi mgeni rasmi katika mahafali ya tano ya shule hiyo,
Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda.
Mgeni
rasmi katika mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius
Kings ya jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha
Mapunda (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na
wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Wahitimu wa darasa la saba Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
SERIKALI inajianda kufanya mabadiliko ya mtaala wa elimu wa
darasa la tatu na la nne ili kukidhi mahitaji ya elimu nchini
ambayo yanabadilika kulingana na muda.
Akizungumza kwenye mahafali ya tano ya Shule ya Awali na
Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es
Salaam, Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Ilala Asha Mapunda,
alisema tayari mitaala ya darasa la kwanza na la pili
imeshabadilishwa.
Mapunda aliwataka wamiliki na waendeshaji wote wa shule
binafsi katika manispaa ya Ilala kuzingatia kwa ukamilifu
taratibu na sheria za nchi katika uendeshaji wa shule binafsi.
“Zingatieni pia mitaala inayotolewa na Serikali.Hivi karibuni
kumekuwa na mabadiliko katika mtaala ya madarasa ya kwanza
na pili, kutakuwa pia na mabadiliko ya mtaala katika madarasa
mengine la tatu na la nne” alisema Mapunda na kuongeza kuwa:
“Hivi ninavyosema kuna baadhi ya walimu wetu wa darasa la
tatu na la nne wako kwenye mafunzo.Lakini nina hakika kabisa
hata shule za binafsi zitapata mafunzo hayo, kwa hiyo wala
msijali.”
Aliwataka wamiliki na waendeshaji wa shule binafsi wasisite
kuwasiliana ofisi ya elimu ya manispaa ya Ilala pindi wanapotaka
ufafanuzi au maelekezo kutoka serikalini yanahitajika na Serikali
itakuwa tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika.
Alisema Serikali kwa ujumla na Manispaa yake inatambua
mchango wa shule za binafsi katika kuendeleza elimu na
inasisitiza na kutia moyo uwekezaji wa sekta binafsi katika
nyanja ya elimu, kwani imedhihirika kwamba shule binafsi
zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya
elimu nchini.
“Serikali kwa upande wake itaendelea kusaidia jitihada hizi kwa
sera na miongozi ambayo imetolewa ili kuboresha mazingira ya
uwekezaji katika sekta ya elimu” alisema Mapunda na kuongeza
kuwa:
Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Machage Kisyeri alisema
mafanikio ya shule hiyo yametokana na filosofia yao ya kuamini
katika kujenga uwezo wa mtoto kimaadili, kinidhamu na umahiri
wa kitaaluma.
“Genius pia tunaamini kuwa kumcha Mungu ni chanzo cha
maarifa yote, hivyo shule yetu imeweka utaratibu mzuri
unaowapa watoto wote wa dini tofauti fursa ya kufanya ibada
pamoja na viongozi wa dini ambao tunafanya kazi nao kwa
karibu sana” alisema Kisyeri.
Naye Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siyame alisema katika mahafali
hayo wanafunzi 65 wanatarajiwa kuhitimu mwaka huu ambapo
kati yao 23 ni wanawake na 42 ni wanaume.
Takwimu zinaonesha ufaulu wa wanafunzi wanaohitimu mitahani
ya darasa la saba kutoka katika shule hiyo umekuwa ukiimarika
kila mwaka ambapo mwaka 2013 wanafunzi wanne kati ya
wahitimu 32 walipata daraja A na mwaka 2015 wanafunzi 40
kati ya walihitimu 57 walipata daraja A.
Aidha udahili wa wanafunzi wa shule hiyo umekuwa ukiongezeka
mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2013 wanafunzi 32
walihitimu na mwaka jana wanafunzi 57 walihitimi huku kukiwa
na mwanafunzi mmoja tu aliyefaulu kwa wastani wa daraja C.
Akizungumzia nafasi ya shule hiyo katika shule bora kwenye
mitihani ya kitaifa, Mkurugenzi Kisyeri alisema shule hiyo ilishika
nafasi ya saba katika mithani ya mwaka 2013 hadi nafasi ya tano
katika mitihani ya mwaka jana katika manispaa ya Ilala.
Akizungumzia umuhimu wa michezo, Mkuu wa shule Siyame
alisema Watanzania wengi hawana mwamko wa michezo, huku
wazazi na wadau wa elimu bado wakiiona michezo kama chanzo
cha mmomonyoko wa maadili na kupunguza morali ya kusoma
shuleni.
“Kwa upande wangu ninaona wakati umefika kwa Watanzania
kubadilika kifikra kwani michezo ni ajira kama zilivyo ajira
nyingine, pia inasemekana sasa hivi michezo ni ajira yenye
malipo makubwa sana kwa hiyo tuwape fursa na tuwawezeshe
watoto wetu kushiriki katika michezo.
Shule ya Genius Kings ilianzishwa mwaka 2008 ambapo baadhi
ya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya
kitaifa ya kumaliza elimu msingi hupatiwa udhamini wa masomo
yao ambapo kwa mwaka huu ni wanafunzi watato
watasomeshwa hadi kidato cha nne.
SHARE


























No comments:
Post a Comment