WENYEVITI wa Halmashauri ya wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam
wamekutana Wilayani Bagamoyo katika Semina maalum ya kujengeana uwezo na
uwelewa ikiwamo kutambua majukumu yao kwa lengo la kuepusha migongano
kati ya Wenyeviti,Watedaji pamoja na Madiwani.
Akizungumza wilayani humo mara baada ya kufungua semina hiyo
Mwenyekiti wa Wenyeviti mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti
wa wenyeviti Wilaya ya Kinondoni Juma Zubery amepongeza hatua ya
wenyeviti wa wilaya ya Ilala kuona kuna umuhimu wa kufanya semina ya
kukumbusha na kuelekezana majukumu ya wenyeviti katika mitaa mbalimbali
ili kuepusha migongano kati yao na watendaji wengine wa Serikali.
Zubery amesema uendeshaji wa Serikali za mitaa una changamoto
kubwa ikiwamo viongozi wengi kushindwa kujua mjukumu yao hali
inayosababisha kutofautiana mara kwa mara miongoni mwao na kufikia hatua
ya mtendaji wa mtaa na mwenyekiti kugombea hata mihuri jambo ambalo
kimsingi linatokana na uelewa mdogo wa kutojuwa mipaka ya kazi zao.
Kwaupande wake Menyekiti wa Wenyeviti katika Manispaa ya Ilala
Ubaya Chuma amewataka wenyeviti hao kuogopa kutumia mihuri ya watendaji
wa mtaa huku akidai kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria na hivyo
kukaribisha migongano miongoni mwao.
Katika Semina hiyo wenyeviti zaidi ya 44 kutoka Halmashuri hiyo
wamekutana huku wakimomba Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuona
umuhimu wa kuandaa mafunzo kama hayo kwa wenyeviti wote wa Serikali za
mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam
Juma Zubery Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua
Semina elekezi kwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa wilaya ya Ilala ambapo
lengo la semina hiyo ilikuwa ni kuwajengea uwezo na uwelewa juu ya
majukumu yao.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mogo, Geoge Mtambalike akitoa
mada ya ulinzi na usalama katika semina hiyo ya wenyeviti wa serikali
ili kujuwa namna ya kuweza kukabiliana na vitendo vya kiarifu katika
mitaa yao.
Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa wilaya ya Ilala,
Ubaya Chuma akiwasilisha mada mbele ya wajumbe ambao ni wenyeviti wa
Serikali za mitaa mbalimbali wilayani humo ambapo alijikita katika kutoa
elimu ya kutambua majukumu yao nakuacha kumbea mihuri huku akidai ni
makossa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kuchukua mhuhuri wa mtendaji wa
mtaa au kata.
Wenyeviti wa Serikali za mitaa mbalimbali kutoka Halmashauri ya
wilaya ya ilala wakisikiliza kwa makini mada ambayo ilikuwa ina tolewa
na mtoa mada,Ubaya Chuma kuhusu wenyeviti hao kuona kwamba wanajukumu
kubwa la kulinda usalama wa maeneo yao ikiwa pamoja na kuimarisha
vikundi vya ulinzi na usalama.
Katibu Tawala wilaya Bagamoyo Mjini Doris Mwakitobe akizungumza
jambo wakati wakufunga semina ya wenyeviti wa serikali za mitaa
mbalimbali wilaya ya Ilala,ambapo katika kufunga semina hiyo aliwataka
kwenda kutumia mafunzo hayo kufanya kazi kwa bidi na kwa kuzingatia
kauli mbiuya rais ya Hapa kazi tu kulia ni Mwenyekiti wa serikali ya
mtaa wa mogo Geoge mtambalike.
Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
SHARE








No comments:
Post a Comment