Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa
Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi
wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi
huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally
Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi
wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua
mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa
Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016. Kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa
Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi
wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi
huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya WaziriMkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa
Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi
wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi
huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally
Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watalaamu wa ujenzi wa mradi wa nyumba
za makazi Magomeni watumie utaalamu wao vizuri na wakamilishe kwa
wakati.
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Novemba 18, 2016) wakati alipokagua
ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na wataalamu kutoka Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu amewataka wataalamu hao waendelee kufanya kazi hiyo kwa kufuata
misingi ya weledi wa taalauma yao kwani Serikali inawaamini. “Muhimu
mjue kwamba mmepewa dhamana hii kubwa ya kukamilisha ujenzi huu ili
wananchi waliokuwa wanaishi hapa waweze kurudi katika makazi yao,”
amesema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA, Mhandisi Edwin Nnunduma
amesema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itahusisha majengo matano ya
makazi. “Kati ya majengo haya matano, manne yatakuwa na ghorofa nane na
moja litakuwa na ghorofa tisa, ambapo wakazi zaidi ya 600 waliokuwa
wanaishi eneo hili tangu zamani watakabidhiwa,” amesema.
Mhandisi
Nnunduma amesema majengo hayo yanajengwa kwa teknolojia ambayo
imezingatia uwezo wa wakazi wake ambapo ina majiko yanayoweza kutumia
kuni na mkaa.
Amesema
mradi huo ambao unajengwa kwa awamu tofauti utahusisha ujenzi wa nyumba
za makazi, maduka makubwa na ya kisasa pamoja na ofisi.
Mhandisi
huyo amesema awamu ya kwanza iliyoanza Oktoba Mosi, mwaka huu inahusisha
ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo
hilo ambayo inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment