Wahitimu Aziza Mkawa na Amina Ally wakimlisha keki mwenzao Eugenia Msahala aliyehitimu juzi chuo kikuu cha Iringa
Wahitimu
wa chuo kikuu cha Iringa Rubeny Nyagawa kulia ,Anna Laiza , Deodatus
Mnyang'ari na Anna Lwanda wakijipongeza kwa keki baada ya kuhitimu
digirii ya biashara na utawala katika chuo kikuu cha Iringa
Na MatukiodaimaBlog
UONGOZI
wa Chuo kikuu cha Iringa (UoI) umepongeza jitihada zinazofanywa na
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli juu ya
uhakiki wa watumishi hewa wenye vyeti feki kwa madai hatua hiyo
ni nzuri itasaidia kupata wataalam wenye sifa sahihi tofauti na
ilivyokuwa awali kuwa na utitiri wa watumishi wasio na uwezo.
Pongezi
hizo zimetolewa jana wakati wa mahafali ya chuo hicho na
mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, askafu wa kanisa la kiinjili la
kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Odenburg Mdegela
alisema kuwa zoezi hilo linapembua mchele na chuya na kuwaacha wale
wenye vyeti halai tu.
Alisema
ilikuwa si sahihi mmoja akae darasani miaka mitatu na mwingine apate
cheti kutoka kariakoo tena kikiwa a ufaulu wa juu kuliko Yule aliyekaa
darasani.
Dkt.
Mdegela alisema watu hawa wanapokutana kazini Yule alipata vyeti bandia
vyenye ufaulu wa hali ya juu anakuwa hajui kazi jambo lililokuwa
likirudisha nyuma maendeleo ya taasisi nyingi na nchi kwa ujumla.
“Uhakiki
wa vyeti unapaswa kuungwa mkono na wadau wote wakiwemo wa elimu kwa
kuwa hali ilikuwa mbaya huku wale wenye vyeti badia vikiwa na ufaulu wa
hali ya juu ilhali hawajui kazi”, alisema Dkt. Mdegela
Aidha
alisema Chuo hicho kinajipanga kuachana na mtazamo uliojengeka kwa muda
mrefu wa kujiendesha kwa kutegemea wafadhili mbalimbali wa ndani na nje
ya nchi pamoja na mikopo ya ada za wanafunzi kutoka serikalini.
Alisema
wanatarajia kuanzisha Asasi itakayokuwa imeungwanishwa na Chuo ambayp
itakuwa ikitoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi ambao wamekwama kupata
huduma hiyo kutoka maeneo mengine.
Kwa
upande wake mkuu wa Chuo hicho, Jaji mkuu mstaafu Augustine Ramadhani
alisema ni vema wahitimu wakawa wazalendo kwa nchi yao na kuitumia elimu
waliyoipata kwa maendeleo ya watanzania wote.
Huku
makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Joseph Madumula alisema mazingira ya
utoaji wa elimu kwa sasa yamekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka
ya nyuma ambapo kulikuwa na Chuo kikuu kimoja cha Dar es Salaam kikiwa
na matawi mawili ya Sokoine na Muhimbili.
Aliongeza
kuwa kwa sasa kuna zaidi ya vyuo vikuu 60 vya binafsi na serikali
lakini idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa haijaongezeka kulingana na vyuo
idadi ya vyuo.
Alisema
wamejipanga kutoa elimu shirikishi ya ujasiliamali kwa wanafunzi wote wa
Chuo hicho ili wakimaliza wasitegemee kuajiriwa tu bali wawe na uwezo
wa kujiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana wengine.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment