Kundi
maarufu linaloipinga serikali ya Cuba limesitisha maandamano yake ya
kila wiki kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na tatu
kufuatia kifo cha Fidel Castro ambaye wao wamekuwa wakimpinga kwa miaka
yote.
Kiongozi
wa kundi hilo la wanawake maarufu kama Ladies in White, Berta Soler,
amesema ametaka kutoa fursa kwa wengine kuomboleza na hivyo
hatasheherekea kifo cha mtu yeyote.
Maandamano hayo ya wanawake ya kila wiki ni kwa lengo la kuwaunga mkono waume zao waliofungwa kwa sababu ya kuipinga serikali.
Kumekuwa
na hali ya simanzi katika mji mkuu wa Havana siku kilipotangazwa kifo
cha Fidel Castro. Mwandishi wa BBC mjini humo amesema watu bado wapo
katika mshtuko.
Baadhi ya raia mjini Havana wanasema wameanza kukubaliana na hali halisi:
Lazaro
Alonso, anasema " Ni vigumu sana kukubali, lakini ndivyo maisha yalivyo.
Tunaendelea kufanya kazi kwa bidii, kusonga mbele, hakuna kitakachozuia
huo mchakato, na tunatahadhari kwamba ndio, iko siku mambo makubwa
yatatokea nchini humu."
Victor
Manuel, naye amenukuliwa akisema "kwetu sisi, kamanda wetu ndio baba wa
familia, baba wa mapinduzi, baba tuliyekuwa nae, ambae siku zote na leo
tunahisi tumempoteza katika maisha yetu."
Leo Jumatatu, Cuba inaanza siku tisa za maombolezo rasmi.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment