TRA

TRA

Tuesday, November 29, 2016

MANUNUZI YA PAMOJA KUPITIA GPSA: SERIKALI YAOKOA BILIONI MOJA KWENYE MAGARI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Na Barnabas Lugwisha
Serikali kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) hivi karibuni imeokoa shilling bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw Jacob Kibona, amewaambia Waandishi wa Habari jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya shilingibilioni 58.1 iwapo kila taasisi ingenunua magari yake.
“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi yapamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” Alisema
Alisema fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya ummana kama vile kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu.
 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) faili lenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza mafaili hayo kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Amesema taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktobamwaka huu, imezikabidhi taasisi za serikali magari ya aina mbalimbali yapatayo 136.

Alisema katika kuhakisha kwamba wanapunguza gharama katika manunuzi, wamekuwa wakinunua bidhaa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja ila inaposhindikana kutokana na sera za makampuni makubwa kuwa na mawakala wa usambazaji wamekuwa wakinunua kwa mawakala hao kwa makubaliano maalum ya kupunguza bei.
Alisema kuwa kazi nyingine muhimu ya taasisi yake ni kugomboa mizigo kupitia bandarini , viwanja vya ndege na mipakani kwa niaba ya serikali ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita waligomboa mizigo yenye thamani ya Shlingi bilioni 62.7.

Alisema mizigo hiyo ilikuwa ni pamoja na vifaa vya mkongo wa taifa, vifaa vya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wizara yaMali asili na utalii.
 
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu pia walikomboa vifaa mbalimbali vya serikali zikiwamo ndege mbili zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada aina ya Bombadier vyote vikiwa na thamani ya Shilingi bilioni 100.97.

Alisema GPSA ina huduma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya taasisi za serikali, kwa kuwa wao wana maghala makubwa katika mikoa karibu yote .

“Hata mkoani Kagera baada ya maafa ya tetemeko la ardhi, maghala yetu yanayotumika kuhifadhi vifaa mbalimbali viliyotolewa kama misaada,”

Pia wana jukumu la kutoa huduma ya mafuta kwa magari yaserikali na kwamba kwamba hadi sasa wamefanikiwa kusimika mfumo wa usimamizi wa mafuta kwa matumizi ya ya serikali na kwamba mfumo huo unaendelea kupanuliwa ili uzifikie taasisi nyingi za umma.
Alizishauri taasisi za umma kuzingatia sheria za manunuzi kwa lengo la kutoa huduma bora na kwa kuhakikisha kuwa vifaa na huduma zinazopatikana zinazingatia thamani halisi ya fedha zinazotumika

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger