TRA

TRA

Monday, November 28, 2016

TANGA YAWATAKA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI INDIA KUWEKEZA ILI KUWEZA KUNUFAIKA KUTOKANA NA UWEPO WA RASILIMALI NYINGI ZILIZOPO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa amewakata wawekezaji kutoka nchini India kuwekeza mkoani humo kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo kilimo, utalii, elimu na Afya ili kuweza kunufaika nazo.

Mwilapwa alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika hotel ya Tanga beach jijini Tanga uliowahusisha wafanyabiashara kutoka India na Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye (katikati) akizungumza jambo na Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kushoto) wakati wa kongamano la wafanyabiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga.  kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi.

Kongamano hilo lilikuwa na lengo lilikuwa ni kushirikisha mawazo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapa ili kufanya uwekezaji ambao utaweza kuleta tija ya kimaendeleo.

Alisema kuwa India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukuza uchumi kwa baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania hivyo uwepo wao katika suala la uwekezaji linaweza kuwa chachu ya kuweza kuinua kasi ya ukuaji wa maendeleo.

   “India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi kwa baadhi ya nchi dunia ikiwemo Tanzania kutokana na hilo niwatake muona namna ya kuwekeza mkoani hapa kwani yapo maeneo mengine mnayoweza kufanya hivyo “Alisema.

Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye.

Awali akizungumza Balozi wa India nchini, Sandeep Arya alisema ujio wa Waziri Mkuu wa India Tanzania umeongeza ari kwa Taifa ilo kuona haja ya kuendelea kuwekeza na kusaidia katika masuala mbalimbali ya afya, Elimu Bishara na Kilimo.

Alisema kuwa soko la India linahitaj bidhaa zenye ubora na rahisi hivyo anaamini kutokana na ushirikiano wa nchi hizi mbili kufanana mahitaji kutakuwepo na fursa kubwa ya muingiliano wa kibiashara ambao utaleta tija na faida kwa pande zote mbili.

Hata hivyo alisema licha kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, matibabu ya kansa lakini wanatoa nafasi 350 za mafunzo nchini india kila mwaka ili kuwapatia nafasi watu kujifunza jinsi India inavyofanya kazi katika shughuli zake za uzalishaji.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini India na
Tanzania wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Thobias Mwilapwa (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara juzi kwenye ukumbi wa hotel ya Tanga Beach Resort.
Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikaribishwa kuzungumza alisema moja kati ya mipango ya Serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli ni kuhakikisha inakuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mwananchi wa hali ya nchi hivyo hakuna haja ya wananchi kukata tamaa.

Nape alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa kuzitumia fursa zilizopo hapa nchini ili kuhakikisha zinaleta manufaa kwa wananchi kwa kukuza vipato vyao na hata kuongeza pato la Taifa. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara. wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger