Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muunngano wa Tanzania Bi Samia Suluhu amewasihi
viongozi wa serikali na wananchi kutumia ndege za Shirika la Ndege
Tanzania(ATC) ili kudumisha uzalendo na kuchangia pato la shirika hilo
kwa lengo la kuhimili ushindani na kukuza uchumi wa nchi.
Ametoa
rai hiyo jijini Dar es salaam alipopewa hati ya kusafiria kupitia ndege
za shirika hilo wakati akisafiri na ujumbe wake kuelekea mkoani Mwanza
kwa ziara ya kikazi.“Napenda
kutoa wito kwa viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutumia
ndege zetu ili shirika letu lifanye kazi vizuri zaidi, kufanya hivi
kutaongeza pato na kukuza uchumi wa nchi ”, amesema Makamu wa Rais.
Ametanabaisha
kuwa kwa kutumia ndege za Shirika la ATC kwa safari za ndani Serikali
itaokoa fedha nyingi zinazotumika kwa kukodi ndege za mashirika binafsi.“Mimi
na ujumbe tumeamua kusafiri na ndege za shirika la ndege Tanzania
kutokana na kubana matumizi, gharama tuliyotumia kwa safari hii ni
shilingi Milioni saba na laki sita ambapo tungekodi ndege binafsi
tungetumia milioni arobaini”, amefafanua Makamu wa Rais.
Kwa
upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa, amempongeza Makamu huyo kwa kitendo cha uzalendo
alichokionyesha na kutaka viongozi wengine wa Serikali na wananchi kwa
ujumla kuiga mfano huo ili kuliinua shirika hilo na kuongeza uchumi.
“Nampongeza
Makamu wa Rais kwa kuamua kutumia ndege za Shirika hili kwa safari za
ndani, kitendo hiki kimeonesha nia ya dhati ya serikali ya kulifufua
shirika hili, naomba wananchi nao waendelee kutumia ndege za shirika
hili katika safari zao za ndani kama alivyofanya Makamu wa Rais”,
amesema Waziri Mbarawa.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandishi Ladislaus Matindi
ameahidi kuboresha huduma katika shirika hilo ikiwemo mifumo ya
kukatisha tiketi ili kurahisisha utoaji wa huduma na kuvutia wateja
wengi kwa lengo la kurudisha hadhi ya shirika.
“Tumeshaanza
mchakato wa kuweka mfumo mpya wa kukatisha tiketi ikiwemo kwa njia ya
kielektroniki kupitia tovuti ya shirika hili ambapo mteja hatalazimika
kufika kwenye ofisi zetu”, amesema Mhandis Matindi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akionyesha
mfano wa hati ya safari ya kuelekea Mwanza kupitia Shirika la ndege la
Tanzania (ATCL), kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiongea
na waandishi wa habari kabla ya kufanya ziara ya kikazimkoani Mwanza
kupitia Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni
kutoka kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa anga katika uwanja wa
Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) wakati alipokagua utoaji wa
huduma uwanjani hapo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni
kutoka kwa wasafiri wanaotumia usafiri waa anga katika uwanja wa
kimataifa wa Julius Nyerere wakati alipotembelea kukagua huduma
zitolewazo uwanjani hapo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni
kutoka kwa wasafiri wanaotumia usafiri waa anga katika uwanja wa
kimataifa wa Julius Nyerere wakati alipotembelea kukagua huduma
zitolewazo uwanjani hapo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza
jambo kwa wahudumu wa ndege katika Chuo cha Shirika la ndege Tanzania
(ATCL) alipotembelea kuona maendeleo ya chuo hicho.PICHA NA BENJAMINI SAWE-MAELEZO
SHARE
No comments:
Post a Comment