Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa nne kulia),
akiteta jambo la Afisa Habari, ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Atley
Kuni (wa tatu kushoto) alipotembelea uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini
Mwanza hii leo ili kujionea zoezi la uwekaji wa nyasi bandia kwenye
uwanja huo.
Waziri
Nhauye ameeleza kuridhishwa na uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja
huo ambapo amewashukuru wadau wote waliofanikisha ukarabati wake
wakiwemo wajasiriamali Jijini Mwanza ambao kodi zao zimesaidia
upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni 190 kutoka Halmashauri ya Jiji
hilo ambazo zilizojumuishwa na dola za Kimarekani Laki Tano zilizotolewa
na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi
huo.
Altaf
Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia
ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Na BMG
Itakumbukwa
kwamba nyasi bandia kwa ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa
muda mrefu baada ya TFF kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi
Milioni 32 hali ambayo ilisababisha utekelezaji wake kusuasua.
Waziri
Nape Nhauye amesema Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali
nchini ikiwemo kushirikiana na makampuni mbalimbali ili kukarabati
viwanja vilivyopo ili Tanzania iwe sehemu bora hata kwa mataifa mengine
kufika kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali hususani ya mpira wa
miguu.
Altaf
Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia
ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Wadau
wa michezo Jijini Mwanza wamefurahishwa na uwekaji nyasi kwenye uwanja
mkongwe wa Nyamagana ambao ulianzishwa mwaka 1945 ambapo wamesema
utaongeza chachu ya ongezeko la mechi za mpira wa miguu Jijini Mwanza
pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato pia.
Uwanja
mkongwe wa Nyamagana sasa unang'aa kwa viwango vingine, ambapo Waziri
Nape amesema anashawishika kuandaa mechi ya kirafiki kati ya timu za
Simba na Yanga zinazoundwa na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, itakayochezewa kwenye uwanja huo.
Itakumbukwa
kwamba Mwaka 1974 timu za Simba na Yanga zilikutana kwenye uwanja wa
Nyamagana, kwenye Fainali ya Ligi ya Taifa ya Soka ambapo Yanga
iliichapa Simba bao 2-1
Mwonekano wa Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuwekewa nyasi bandia
SHARE
No comments:
Post a Comment