
Mkurugenzi
wa Michezo, Yusuph Omari; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi kwa kushirikiana na Makamu Rais wa Kamati ya
Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau leo Jumatatu Januari 30, kwa
pamoja watazindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki
michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan.
Uzinduzi
wa kampeni hizo unaopewa jina la ‘The Road to Tokyo 2020’ utafanyika
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam saa 5.00 asubuhi ambako wadau na
wafamilia wa mpira wa miguu wanakaribishwa.
Tayari
timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro
Warriors’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza
mechi za kufuzu fainali hizo za za Olimipiki.
Kambi
hiyo imepigwa kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.
Tanzania
haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu
jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu
kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),
kufanikisha mipango na taratibu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment