Mhamiaji mwanamke na mtoto waliokolewa na kikosi cha walinzi cha pwani ya Libya, wakiwasili Februari 5, 2017 mji wa Tripoli.
Wahamiaji 1,500 wamrokolewa mwishoni mwa wiki hii katika pwani ya
Libya, idadi ambayo ni kubwa katika msimu huu wa baridi ambapo idadi
imepungua kutokana na hali ngumu ya hali ya hewa.
Idadi hii, iliotolewa na walinzi wa
pwani ya Italia ambao wanaratibu shughuli katika eneo hilo, imefikia
sasa zaidi ya wahamiaji 4,500 waliokolewa tangu siku ya Jumatano.
Siku ya Jumapili, wahamiaji 900 ambao
walikua wakisafiri katika boti tatu wameokolewa katika bahari ya
Mediterranean na meli ya kikosi cha jeshi la majini cha Uhispania
(Canarias), na meli zingine za kawaida.
Siku moja kabla, wahamiaji
600waliookolewa bila tatizo lolote wakati wa shughuli tisa tofauti
zilizoendeshwa na Diciotti, meli ya kikosi cha walinzi wa pwani ya
Italia.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana
mjini Malta, waliahidi siku ya Ijumaa kusaidia nchi ya Libya kupambana
dhidi ya wapita njia, lakini mashirika mengi ya kimataifa na mashirika
yasiyo ya kiserikali yalionya dhidi ya hatua zitakazochukuliwa.
Italia na Libya kwa upande wao,
walisaini mkataba wa makubaliano unaoelezea uimarishaji wa mipaka yao
ili kufanikisha, kwa msaada wa Umoja wa Ulaya, kupunguza wingi wa
wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini kuelekea nchini Italia.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment