Mamia ya
waandamanaji wameandamana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK
wakipinga sera ya uhamiaji ya Donald Trump inayopiga marufuku wahamiaji
kuingi anchini Marekani, Januari 28, 2017.
Agizo la
Donald Trump ambalo linapiga marufuku raia kutoka mataifa mengi ya
Mashariki ya Kati kuingia nchini Marekani limezua hali ya sintofahamu
katika makampuni ya Silicon Valley. Makampuni ya teknolojia mpya
yanaajiri idadi kubwa ya vijana wenye vipaji kutoka katika ukanda huo.
Waajiri
wa Silicon Valley wamechukua uamuzi wa kupinga dhidi agizo la rais Trump
ambalo linapiga marufuku wahamiaji nchini Marekani. Hata kampuni ya
Twitter, moja ya mitandao ya kijamii anayotumia Rais wa Marekaniimesem
ainaunga mkono wahamiaji.
Wkurugenzi
Wakuu wa Apple, Facebook, Netflix, Google na Microsoft wanakubaliana
katika kulaani kikwazo hiki kwa kuajiri wahandisi wengi katika sekta hii
kutoka nchi zilizolengwa na agizo la rais Donald Trump.
Apple,
kampuni ilioanzishwa na Steve Jobs, mtoto wa mhamiaji kutoka Syria,
"haitokuwepo bila wahamiaji," amesema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,
Tim Cook. Mmiliki wa kampuni ya Netflix , kwa upande wake ametoa wito wa
kulinda maadili ya Marekani ya uhuru na nafasi. "Hatua za Trump
zinaathiri wafanyakazi wa kampuni ya Netflix duniani kote ... Ni wakati
wa kujiunga pamoja na kulinda maadili ya Marekani ya uhuru na nafasi,"
Reed Hastings ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook.
Microsoft,
kwa upande wake, inasema kwamba hali hii itaizuia kujaza nafasi zote
zilizo wazi katika timu za utafiti na maendeleo. Takriban wafanyakazi
187 wa kampuni ya Google wanaathirika na vikwazo hivi vipya, amesema
kwenye barua pepe ya kamupuni hiyo Sundar Pichai, Mkurugenzi mkuu wa
Google.
Eloni
Musk, mwanzilishi wa kampuni ya Tesla na SpaceX ambaye hivi karibuni
alikutana na Donald Trump, amebaini kwenye Twitter kwamba "marufuku ya
jumla kwa wananchi kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kuingia nchini
Marekani si njia bora ya kukabiliana na changamoto " zinazonatokea.
Kwa
upande wa mmiliki wa Microsoft, mwenye asili ya India, amesema, kama
wmhamiaji na kama Mkurugenzi Mkuu, athari chanya ya uhamiaji.
Itafahamika
kwamba agizo la kupiga marufuku raia kutoka nchi saba za Kiislamu
kuingia nchini Marekanililisababisha mikusanyiko na maandamano ya hasira
nchini kote, siku moja baada ya krais Donald Trump kutia saini kwenye
agizo hilo. Zaidi ya watu 2000 walivamia na kuandamana katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa John Fitzgerald Kennedy, huku wakidai kuachiwa
huru kwa watu waliozuiliwa kwenye idara ya Forodha. Wakati huo huo, jaji
wa mjini New York aliomba kuachiliwa kwa wasafiri wote waliokua na visa
halali.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment