Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa akizungumza juu ya Bonanza hilo
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa habari Sanaa, utamaduni na Michezo, Nape Nnauye anataraji kuongoza Bonanza
la mazoezi na upimaji afya February 18 mwaka huu ulionadaliwa na Chama
cha maofisa mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na jukwaa la
wahariri Tanzania na Dar es Salaam City Press Club.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msemaji wa chama TAGCO,
Abel Ngapemba ametaja kuwa lengo la Bonanza hilo ni kuhamasisha
wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya kama
ilivyozoeleka kwa kuunga mkono kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rais
Mama Samia Suluhu Hassan.
“washiriki
wa bonanza hili ni pamoja na maofisa mawasiliano wa Serikali na wasekta
binafsi ,Wahariri , Wahandishi wa habari na Bloggers na wananchi kwa
ujumla kwa kuongozwa na Waziri Nape Nnauye na kuhudhuliwa na viongozi wa
Wizara ya afya na ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto” amesema Abel.
Ametaja
kuwa mbali ya mazoezi taasisi zitakazo shiriki kutoa huduma siku hiyo
ni pamoja na Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Saratani ya
Ocean Road,Hospitali ya Sanitas,CCP Medicine Kinyerezi na Mfuko w Bima
ya Afya (NHIF), Chama cha madaktari wa meno Tanzaniana tasisi ya
wagonjwa wa mifupa MOI.
Abel
ametoa wito kwa wahariri wa vyombo vya habar, waandishi wa habari ,
Bloggersna maofisa mawasiliano Serikalini, mashirika binafsi na tasisi
za kimataifa kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment