TRA

TRA

Tuesday, February 28, 2017

DC HAPI ATOA SIKU SABA KWA WACHIMBAJI WA KOKOTO KATIKA ENEO LA BOKO KUPISHA UJENZI WA DAMPO LA KISASA.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Na Anthony John Glob ya Jamii.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Alli  Hapi ametoa muda wa siku saba kwa wachimba kokoto wa eneo la Boko chama kuondosha mawe yao yaliyopo kwenye eneo hilo, ili kupisha ujenzi wa dampo la kisasa.

Kauli hiyo ya DC Hapi imekuja baada ya kutembelea na kukagua eneo hilo ambalo awali wachimbaji wake walipewa amri ya kutokuendelea na uchimbaji wa kokoto, lakini baadhi wamekaidi amri hiyo na kuendelea.

Akielezea zaidi Hapi amewataka kutokuendelea kuchimba na hasa katika kipindi hiki cha mvua, kwani wanaweza kujisababishia madhara ya kufukiwa na kifusi na kupoteza uhai.

Amesema amewaelekeza maafisa mazingira na mipango miji wa manispaa waunde timu ,waangalie uwezekano wa kuweka dampo kwenye eneo hilo, kwani eneo la dampo lililopo ni moja Pugu Kinyamwezi, ambako ni mbali.

Aidha amesema dampo hilo lifanywe la kisasa ili uwe mradi ambao utasaidia kuingiza mapato kwa manispaa.

Aidha HAPI ameeleza kuwa pindi eneo hilo litakapoanza kutengenezwa watu waliokuwa wakichimba hapo waandae orodha ya majina ili mawe yatakayotolewa hapo wapewe wao.

Kwa upande wake afisa mazingira wilaya ya kinondoni Mohamed Msangi amesema, eneo hilo likifanywa dampo litarahisisha utupaji taka kwa wakazi wa eneo la boko, mabwepande, bunju,  kawe na mwenge.
 Eneo linalochimbwa kokoto na baadhi ya Wakazi wa Boko chama,ambalo kwa sasa utaratibu wake umesitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh.Ally Hapi
 Mkuu wa wilaya  ya Kinondoni Ally Hapi akiwa na wakazi wa Boko chama katika eneo la uchimbaji wa kokoto
  Mkuu wa wilaya  ya Kinondoni  Ally Hapi  akizungumza  na watendaji wa Kata pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa jana katika Ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Bunju katika ziara yake ya siku kumi.
 Wenyeviti wa Serikali za mitaa na watendaji katika Kata ya bunju  wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kinondoni  Ally Hapi jana katika ziara yake.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger