Na Jumbe Ismailly -HANANG .
ALIYEKUWA
diwani wa kata ya Gihandu,wilayani Hanang,Mkoani Manyara kwa tiketi ya
Chama cha ACT Wazalendo,Mathayo Samuhenda amejiuzulu udiwani wa kata
hiyo na kujiunga na Chama Chama Mapinduzi (CCM)
Akitangaza
azma yake hiyo ya kujiuzulu katika nafasi yake ya udiwani wa kata hiyo
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Gihandu,Samuhenda alisisitiza kwamba aliamua kujiuzulu na kuwaacha
wapiga kura wake siyo kwa njia ya ukatili bali alifikia maamuzi hayo kwa
lengo la kuwaunganisha wananchi wote wa kata hiyo.
Aidha
alifafanua kwamba katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa wananchi
wa kata hiyo wana matatizo ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na
salama kutokana na wanasiasa kutumia mtaji huo kuomba kura.
“Inatosha
wanasiasa sisi tutumie shida ya maji ili tuoate kura
tuondoke,inatosha..na watu wa Gihandu nawaomba sana hiyo ikiletwa kama
sehemu ya mnada mzuri tu wa mtu kujinadi mkataeni inatosha tumeumia vya
kutosha.”alisisitiza Samuhenda.
Hata
hivyo diwani huyo aliyejiuzulu aliweka bayana kwamba umefika wakati sasa
kwa wanasiasa kubadili ajenda za kupatia kura za Gihandu na isiwe
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwani hiyo sasa imekuwa ni
kejeli
Akimpokea
diwani huyo,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu alikemea tabia
ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoendeleza makundi licha ya kuwa
hivi sasa siyo wakati wa kumpeni na badala yake aliwataka kuvunja
makundi hayo na kusisitiza juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
kwenye maeneo yao.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo alisisitiza pia kwamba suala la kuvunja makundi
siyo la hiyari bali ni la lazima kutokana na makundi hayo baadhi ya
wanachama mchana wanakuwa CCM huku usiku wanatumikia Vyama vya upinzani.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Hanang,Methew Darema alimpongeza diwani huyo kwa
kitendo chake cha ujasiri cha kujiuzulu nafasi aliyokuwa nayo pamoja na
kwamba ni hivi karibuni alitembelewa na kiongozi wake wa kitaifa kwa
lengo la kuhamasisha watu kujiunga na chama hicho.
Kwa
upande wake baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Gihandu,Stephano Ngudu
alisema mwaka 2008 kila mwananchi alichangia shilingi 86,500/= kwa ajili
ya ujenzi wa shule ya sekondari na Hosteli mbili,lakini mpaka leo
hakuna ujenzi wowote wa majengo hayo uliokamilika na fedha walizochanga
hawajarudishiwa.
Ni
Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,DK.Mary Nagu (wa kwanza kutoka
kushoto) akimpongeza aliyekuwa diwani wa Kata ya Gihandu,Mathayo
Semuhenda mara baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu akipokea kadi ya Chama Cha ACT
Wazalebdo kutoka kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo
Semuhenda.
Aliyekuwa
diwani wa kata ya Gihandu kwa tiketi ya ACT Wazalendo,MATHAYO SEMUHENDA
akipokea kadi ya CCM baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
baadhi
ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya na Mkoa wa Manyara
wakishiriki kikamilifu pamoja na wanachama wapya kula kiapo cha uadilifu
baada ya kuwakabidhi kadi za chama wanachama wapya wa chama hicho.
Aliyekuwa
diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda akila kiapo cha uadilifu
mara baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi(ccm)
SHARE
No comments:
Post a Comment