Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekabidhi
hati miliki za ardhi 1,361 kwa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo
wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Waziri
Lukuvi amegawa hati hizo na kuwasisitiza wananchi wa wilaya ya Mvomero
kuhakikisha wanapata hati za umiliki wa ardhi pamoja na kuwataka
viongozi wa vijiji kote nchini kuhakikisha wanakuwa na mpango wa
matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji
kuendelea katika maeneo yao.
Pia
amesema ili mwananchi aweze kujikimu kimaisha ahakikishe anazitumia
hati miliki hizo za kimila kujiletea maendeleo na anaweza kuomba mkopo
benki kwa kutumia hati hiyo ili kuendesha shughuli zake za kujipatia
kipato kupitia eneo analomiliki kisheria.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amewataka wananchi
kuzitunza hati hizo walizokabidhiwa na kuyatumia mashamba yao
waliyomilikishwa kwa kuyalima na sio kuyauza au kukodisha kwa watu
wengine na wao kubaki masikini.
Waziri
Lukuvi pia alimtaka Mkuu wa mkoa wa Morogoro ayaainishe mashamba
mengine makubwa yasiyoendelezwa na kugeuka kuwa mashamba pori ili
amshauri Rais kuyafutia umiliki wa mashamba hayo na kurudishwa kwao ili
kuweza kuwapa kaya maskini ambazo zinaishi katika maeneo ya hayo.
Kazi
hii ya upimaji wa maeneo na kutoa hati kwa wananchi ni katika mpango wa
nchi wa matumizi bora ya ardhi,ambapo serikali imechangua Mkoa wa
Morogoro kuwa wa Mfano katika upimaji wa ardhi na utahusisha nchi nzima
kwa wapimaji wa ardhi kutumia vipimo vya kisasa zaidi ambavyo kwa kiasi
kikubwa vipimo hivyo vitaweza kupima ardhi kwa kipindi kifupi na kila
mtu kumiliki kipande cha eneo lake.
Lukuvi
alisema kuwa wakati wa kampeni mwaka 2015,Rais Dkt. John Magufuli
alihaidi wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika
maeneo yote ya nchi kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa, na kwa
miaka mitano takribani vijiji 7,500 vitapimwa kwa kupangwa kila
halmashauri 25 ambapo na kila mwaka vitapimwa vijiji 1,500 na kutoa
hati. Alisema kuwa zoezi la upimaji linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya
utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika
kuondoa migogoro inayojitokeza.
Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Ardhi)
Mzee
Ali Juma mkazi wa kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro
akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Lukuvi kumuwezesha kupata hati ya kumuliki ardhi yake ambayo amekuwa
nayo kwa miaka mingi bila kupewa hati hiyo, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa
ya Mipango na Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Dkt. Stephen Nindi
anayemsaidia kwa kumshika mkono.
Bi.
Zaina Hussein mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero mkoani
Morogoro akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
Bibi.
Magret Hamis mkazi wa kijiji cha Hembeti akipokea hati ya kumuliki
ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
Baadhi
wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani
Morogoro wakiwa hati zao za kumuliki ardhi mbele Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Dkt. Stephen Kebwe.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na
wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo na kuwataka wahakikishe
wanazitumia hati miliki hizo za kimila kwa kujiletea maendeleo.
Baadhi
wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani
Morogoro wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro Bwana Limbena
Madela akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi kuwezesha wakazi wa kijiji chake kupata hati miliki hizo
za kimila.
SHARE
No comments:
Post a Comment