Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeanza kutekeleza kwa vitendo
Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na
Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI
alipotembelea Tanzania kwa mwaliko wa Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mnamo mwezi Oktoba 2016.
Katika
kutekeleza makubaliano hayo, ujumbe wa TADB ukiongozwa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Francis Assenga na Mkurugenzi wa Hazina na
Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru upo nchini Morocco, pamoja na mambo
mengine kuainisha maeneo ambayo Benki hiyo itashirikiana na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM) na kuwekeana mikakati ya
utekelezaji.
Kwa
mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo
ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo
Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TAD, Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa na
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru (Watatu
kushoto) wakiwa na wenyeji wao Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco
(GCAM).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw.
Francis Assenga (wa pili toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na
mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit
Agricole) Bw. Jamal Eddine Wl Jamali (Katikati). Wengine ni Mkurugenzi
wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB Bw. Albert Ngusaru na Wakurugenzi
wawili wa Benki ya Credit Agricole Bi. Dkhil Mariem (Kushoto) na Bi
Leila Akhmisse (Kulia).
Ujumbe
wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ukipatiwa maelezo juu
ya miradi ya kilimo inavyoendeshwa nchini Morocco wakati Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga (Mwenye Kaunda Suti) na
Bw. Albert Ngusaru Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha (Mwanye
Daftari) walipotembelea Morocco wiki hii kuanza utekelezaji wa Mkataba
wa Ushirikiano kati ya TADB na GCAM.
Ujumbe
wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ukipatiwa maelezo juu
ya miradi ya kilimo inavyoendeshwa nchini Morocco wakati Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga (Mwenye Kaunda Suti) na
Bw. Albert Ngusaru Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha (Mwanye
Daftari) walipotembelea Morocco wiki hii kuanza utekelezaji wa Mkataba
wa Ushirikiano kati ya TADB na GCAM.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Francis
Assenga (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Credit
Agricole na Tamwil El Fellah wakati walipokagua miradi mbalimbali ya
kilimo na ufugaji katika vijiji vya mji wa Khemisset nchini Morocco
jana. Kulia kabisa ni Bw. Albert Ngusaru ambaye ni Mkurugenzi wa Hazina
na Utafutaji Fedha wa TADB.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw.
Francis Assenga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole) Bw.
Jamal Eddine W. Jamali (Katikati). Kulia ni Mkurugenzi wa Hazina na
Utafutaji Fedha wa TADB Bw. Albert Ngusaru.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Francis Assenga (Kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji
Fedha wa TADB Bw. Albert Ngusaru (Kulia) walipotembelea Benki ya
Kilimo ya Morocco (Credit Agricole).
SHARE
No comments:
Post a Comment