Katibu wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Miembeni lililopo
Kata ya Manzese,Fatuma Mohamed (kulia) akishirikiana na wanachama wa
chama hicho kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mtaa wao kwa ajili
ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM)wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Tawi la Miembeni lililopo Kata
ya Manzese wakishirikiana na wafanyakazi wa hospitali ya Mtakatifu
Monica kuweka taka kwenye sehemu ya kuwekea uchafu kama ishara ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA
…………………..
NA ELISA SHUNDA,DAR
WITO umetolewa kwa wanawake kuwa
mfano wa kuigwa kwa jamii inayowazunguka katika ufanyaji wa usafi katika
mazingira wanayoishi ili kujikinga na magonjwa ya milipuko na
yanayosababishwa na mazingira ya uchafu ukiwemo ugonjwa wa
Kipundupindu,kuhara na Malaria.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja
wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Mtaa wa Miembeni
lililopo Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam jana,Fatuma Mohamed wakati
akizungumza na waandishi wa habari ambapo waliadhimisha siku ya
wanawake duniani kwa kufanya usafi katika maeneo ya mtaa wao ikiwemo
eneo la ofisi za chama za mtaa huo pamoja na Hospitali ya Mtakatifu
Monica iliyopo eneo la Manzese Darajani.
“Leo sisi wanachama wa chama cha
mapinduzi (CCM) UWT tawi la Manzese Miembeni tumejitokeza kufanya usafi
katika mitaa ya eneo letu hili la Miembeni,ofisi za chama chetu za tawi
pamoja na Hospitali ya Mtakatifu Monica ili kuonyesha mfano na
kuwahamasisha wakinamama wenzetu kufanya usafi kwa kujitolea wenyewe
bila ya kushurutishwa ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi na milipuko
kama ugonjwa wa kipundupindu,kuhara hata na Malaria yanayotokana na
wadudu wanaozaliana sehemu za mitaro isiyotembea na takataka zinazokaa
kwa muda mrefu hivyo tumejitolea leo kufanya usafi ili mtaa wetu uwe
mfano wa kuigwa na mitaa mingine”Alisema Mohamed
Aidha Mohamed alisema kuwa
wanaendelea kuhamasisha wananchi wa mtaa wao na kata ya Manzese kwa
ujumla kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka lakini pia ni
wajibu kwa kila mtu kufanya usafi katika eneo lake pamoja na kutosahau
siku ya juma la mwisho wa mwezi lililowekwa na Rais Dk.John Magufuli la
kufanya usafi katika mazingira yao.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa
Tawi hilo,Hanifa Mkura alisema kuwa ni kweli kuna baadhi ya wananchi
hata wakinamama wamekuwa wagumu wa kushiriki kufanya usafi katika
mazingira yao kutokana na hali jinsi ilivyo kuwa ngumu wanakuwa
wanajikita kufanya biashara zao ili wajipatie kipato lakini wao kama
wakinamama watawashauri wapange siku katika wiki wafanye usafi kwenye
mazingira yao yanayowazunguka.
SHARE
No comments:
Post a Comment