Mwanamuziki wa
nyimbo za reggae nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama
Bobi Wine, anaapishwa leo kama mbunge wa eneo la Kyadondo East.
Alisema kuwa anaingia bungeni kama kiongozi na wala si mwanasiasa, kwa mujibu wa gazeti la New Vision.
Chama tawala NRM na upinzani wamekuwa wakimtaka Wine ajiunga na mmoja wao.
Picha ya Wine akimsalamia Rais Museveni wakati wa misa ya mfanyabiashara mmoja ilikosolewa na baadhi ya wafuasi wake katika mitandao.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment