Afrika ni
miongoni mwa bara lenye nchi nyingi maskini duniani lakini hii inaweza
kukushangaza kwani kuna baadhi ya nchi zinatajwa kuwa na ndege za Rais
zenye gharama kubwa ukilinganisha na ndege zinazomilikiwa na Marais wa
nchi zilizoendelea kama Portugal.Leo
nimekutana na hii list ya Marais kumi kutoka Afrika wenye ndege za
kisasa na zenye gharama zaidi barani Afrika hadi kufiki december 2016.
1:Morocco Boeing (747-400)
Hii ni
ndege ya Mfalme wa Morocco inatajwa kuwa ndiyo ndege yenye gharama
kuwahi kumilikiwa na kiongozi yoyote barani Afrika ambapo ina thamani ya
zaidi ya dola milioni 450 ,ndege hii ina vyumba vitano va kulala,ukumbi
wa mikutano na ukumbi wa kuangalia movie.
2: Zimbabwe (Boeing 767)
Licha ya
Zimbabwe kuwa na hali mbaya ya kiuchumi lakini ndege ya Rais wa nchi
hiyo ni ndege ya pili kwa kuwa na gharama barani Afrika ambapo ina
thamani ya dola milioni 400 ina speed ya 858 km kwa lisaa na kuifanya
kua moja ya ndege zenye kasi sana duniani.
3:Nigeria (Boeing 737)
Nigeria
imeshika namba tatu kwa kuwa na ndege ya Rais yenye gharama barani
Afrika ambapo ina zaidi ya thamani ya dola milioni 390.
4:Algeria (A340-500)
Ndege hii
inayotumiwa na Rais wa Algeria ina engine zaidi ya nne,ina uwezo wa
kusafiri angani kwa masaa 24 bila kutua ina vyumba maalum vya kupumzika
na ukumbi wa mikutano.
5:Libya (A340)
Licha ya
changamoto za kisiasa zilizopo Libya lakini nchi hii inatajwa kuwa na
ndege ya Rais yenye gharama kubwa ambapo ina vyumba vya kulala,kumbi za
mikutano ,jiko la kupikia na ukumbi wa sinema.
6:Egypt (Air Bus A340)
Egypt
inatajwa kama nchi yenye ndege ya Rais ya gharama zaidi Afrika ambapo
inavifaa maalum ambapo zitazuia ndege hii kusimama kwenye sehemu za
hatari kama baharini au kwenye milima.
7:Ghana (Falcon 900 Ex Easy)
Ndege hii inatajwa kuwa na gharama ya dola milioni 37 na inauwezo wa kuwa angani bila kutua kwa masaa 13 .
8:Kenya (Fokker 70)
Hii ndiyo
ndege maalum ya Rais wa Kenya ilinunuliwa mwaka 1995 inauwezo wa kubeba
abiria 25 pia inauwezo wa kusafiri kwa 845 km kwa saa.
9:South Africa (Boeng 747)
Ndege hii ina uwezo wa kubeba watu 30 ina kumbi ya mikutano inayoweza kuchukua watu nane na ina vyumba vya kulala .
10:ANGOLA (EMBRAER ERJ-135)
Ndege hii
ya Rais wa Angola inashika namba kumi kwenye list ya ndege za Marais za
kisasa na zenye gharama barani Afrika ambapo ina speed ya 834 km kwa
saa moja .ndege hii ina vyumba vya kulala,sehemu za kulia chakula na
kumbi za sinema.
SHARE
No comments:
Post a Comment