Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw.
Godwin Kunambi (wapili kushoto) hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/=
kwa ajili ya vijana kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji
Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18,
2017. Wanne kushoto ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu
Wziri wake, Anthony Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ,
Christina Mndeme na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na
Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu
wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha
kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla
ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili
18, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (picha na Ofiai ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee Maarufu wa Dodoma, Job
Lusinde baada ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya
serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wengine
pichani kutoka kulia ni Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, AjiraKazi, Jijana, ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP, Bw. Sabasaba Moshingi akizungumza kwa
niaba ya viongozi wa Mifuko ya Uwezeshaji ya Serikali katika maonyesho
ya mifuko hiyo yaliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye
uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipofungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi
ya Serikali kwenye uwanja wa Uhuru mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya
serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa
mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya
serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa
mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na
Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu
wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha
kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla
ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili
18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua maonyesho ya
Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa
mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki
na Kati, Bw. Michael Christian cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya
Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho
hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na
Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Bi. Evelyne Mandenje amabaye ni mmoja
wa wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya TIB
wakati alipotembelea banda la wasindikaji vyakula kabla ya kufungua
Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa
Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta
Tanzania (TPB) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho
ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye
uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakijadili
jambo katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali
yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma
Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa Benki ya TIB,
Kenneth Lusesa(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amelitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC), lianze kufanya tathmini ya kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko
yote ya uwekezaji nchini ili kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi
kama ilivyokusudiwa.
Pia
amelitaka baraza hilo lifanye tathmini kuhusu namna ya kuunganisha
mifuko hiyo bila ya kuathiri majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa
kwake, ili inayofanya kazi zinazofanana iunganishwe .
Ametoa
agizo hilo leo (Jumanne, Aprili 18, 2017) wakati akifungua maonesho ya
mifuko ya uwezeshaji katika uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma. Amesema
uzinduzi wa maonesho hayo ni fursa nzuri kwa wananchi kuweza kudadisi
kuhusu huduma zitolewazo na Mifuko hiyo na kutoa ushauri, ili kuboresha
huduma.
“Lengo
ni kuwa na Mifuko michache, lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika,
ambao ni wananchi. Nitafurahi kupata taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi
Mei, 2018,” amesema.
Aidha,
Waziri Mkuu amesema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa
na Serikali yanalenga kuwawezesha Watanzania wengi wafanye shughuli za
kujiongezea kipato bila kusumbuliwa na baadhi ya Watumishi wasio
waadilifu.
Ameongeza
kuwa “uwezeshaji wananchi kiuchumi ni jambo ambalo lipo kwenye Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango
wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.
Amesema
kuwawezesha wananchi kiuchumi, sio ubaguzi wala upendeleo, bali ni
jitihada za makusudi za kuwashirikisha wananchi walio wengi ambao kwa
sababu za kihistoria, wamejikuta wakiwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi,
hivyo kubaki kwenye hali duni jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na
usalama wa nchi.
Waziri
Mkuu amesema jitihada za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizoanza tangu
Serikali ya Awamu ya Kwanza na kuendelezwa na awamu zote zilizofuata,
ambapo kwa sasa kuna mifuko 19 ya kuwezesha wananchi kiuchumi.
Amesema
mifuko hiyo imesaidia upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na
kupunguza kiwango cha umaskini nchini. “Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko
hiyo kwa pamoja ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni
1.759 kwa wajasiriamali 400,000.
Awali
Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng` Issa alisema maonesho hayo ya siku
nne yatawezesha kuwaongezea wananchi uelewa juu ya shughuli zinazofanywa
na mifuko ya uwezeshaji.
Amesema
kati ya mifuko 19 ya uwezeshaji mifuko 13 imeweza kushiriki katika
maonesho hayo ya kwanza kufanyika nchini, ambapo kauli mbiu ya maonesho
hayo ni “Wezesha wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na
Tanzania ya viwanda”
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank PLC, Bw. Sabasaba Moshingi
aliyezungumza kwa niaba ya washiriki alisema madhumuni ya maonesho hayo
ni kukuza uelewa juu ya uwepo wa mifuko ya kuwezesha wananchi kiuchumi
na fursa zitolewazo na mifuko hiyo.
Pia
kuhamasisha wananchi juu ya kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba na
kuwekeza katika miradi yenye kuleta faida pamoja na uanzishwaji na
uimarishwaji wa vikundi na miradi ya kiuchumi ili kuunganisha wananchi
na fursa za huduma ya mikopo, mafunzo na huduma nyingine zinazotolewa na
mifuko hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment