NA
K-VIS BLOG
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Abdulrahman Kinana, yuko salama na
anaendelea vizuri na mapumziko, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi,
Humphrey Polepole, amewaambia waandishi wa habari mkoani Arusha Mei 5,
2017.
Polepole
ameyasema hayo wakati akikamilisha ziara yake ya kikazi mkoani humo. “Nimezungumza
naye jana, na ameniambia anaendelea vizuri, yuko madhubuti kabisa kuliko jana..”
alisema Polepole.
Polepole
amefafanua kuwa, pamoja na ushiriki wake katika shughuli na mikutano mbalimbali
ya chama ikiwemo ule mkutano mkuu maalum wa CCH uliofanyika mjini Dodoma, afya
ya Katibu Mkuu Kinana haikuwa nzuri na hivyo iliamuliwa apelekwe nje ya nchi kwa
matibabu.
“Na
anaporejea mgonjwa anapotoka hospitali huwa hakimbilii kazini, shambani moja
kwa moja inashauriwa kitaalamu achukue muda kupumzika ili kuimarisha afya yake,
na jana tumeongea nae na anaendelea vizuri.” Alitoa hakikisho Polepole.
Kinana
amekuwa haonekani hadharani kwa muda sasa, tangu kumalizika kwa mkutano mkuu
maalum wa CCM mjini Dodoma kiasi cha miezi miwili iliyopita.
SHARE
No comments:
Post a Comment