TRA

TRA

Saturday, July 22, 2017

JE, UNAFAHAMU HISTORIA YA MUADHAMA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO? SOMA HAPA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 
Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi leo muda mfupi kabla ya kuanza kwa sherehe kutimiza miaka 25 kama kiongozi wa Kiroho katika kanisa la Katoliki jimbo Kuu la Dar es salaam katika kanisa la St. Joseph.
 
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo ni kardinali wa pili kutoka Tanzania, akiwa kateuliwa mara baada ya kifo cha Muadhama Laurean Rugambwa, aliyekuwa kardinali wa kwanza kutoka kusini kwa Sahara. 
 
Alizaliwa kijiji cha Mwazye, mkoani wa Rukwa, tarehe 5 Agosti 1944. Baada ya masomo ya ngazi mbalimbali, alipewa upadrisho mwaka 1971 na askofu Charles Msakila wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, akasoma teolojia ya maadili huko Roma, Italia, akijitwalia digrii ya udaktari mwaka 1977.
Kisha kufundisha somo hilo kwa muda mfupi kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa wa Tabora), baadaye 
alichaguliwa kuwa gombera wa seminari kuu ya Segerea hadi mwaka 1983. 
Aliteuliwa askofu wa Nachingwea tarehe 11 Novemba 1983, akapewa daraja takatifu hiyo na Papa Yohane Paulo II tarehe 6 Januari 1984. 
Tarehe 17 Oktoba 1986 alihamishiwa jimbo jipya la Tunduru-Masasi. Tarehe 22 Januari 1990 alifanywa askofu mwandamizi wa Dar-es-Salaam na mwaka 1992, ambapo Kardinali Laurean Rugambwa alipojiuzulu, akawa askofu mkuu.
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo  aliteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa kardinali tarehe 21 Februari 1998, akikabidhiwa parokia ya Nostra Signora de La Salette mjini Roma. 
Pamoja na majukumu mbalimbali katika idara za Papa, tangu mwaka 2007 hadi 2013 alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika na Madagaska.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger