TRA

TRA

Saturday, May 20, 2017

MKUU WA MKOA MARA WAANDISHI MKO SALAMA FANYENI KAZI KWA WELEDI.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa akiongea na waanadishi wa Habari Mkoa wa Mara katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo ufanyika May Tatu kila Mwaka lakini Klabu ya Waandishi Mkoa wa Mara wameadhimisha jana katika Ukumbi wa Mativilla Beech Mjini Musoma  na Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.


Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) Mugini Jacob akiongea na wanachama wa klabu hiyo  pamoja na wadau wa habari katia Maadhimisho ya siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo Mkoa wa Mara sherehe hizo zimefanyika jana katika ukumbi wa Mativilla Beech Mjini Musoma na Mgeni rasmi akikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa.

Sherehe hizo za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ufanyika May Tatu kila Mwaka.

Mwenyekiti MRPC akiongea na Vyombo vya habari




Kushoto ni Afida Mahusiano kampuni ya  AKO Dickson Christopher kulia ni Meneja PSPF Mkoa wa Mara  Deogratias Njuu wakiwa katika mkutano huo

Mkutano unaendelea.


Mwandishi wa Habari RFA Ahamad Makongo akiuliza Swali

Makamu Mwenyekiti wa Tarime Teachers SACCOS Mwl Johnson Maiga akiongea na Wadau wa Habari pamoja an waandishi katika maadhimisho hayo.

Meneja PSPF Mkoa wa Mara Deogratias Njuu akiongea na waandishi wa habari pamoja na Wadau wa Habari.


Afisa Mahusiano kampuni ya AKO Dickson  Christpher akiongea na wadau pamoja na Waandishi wa Habari.

Mwandishi wa Habari kampuni ya Mwanachi Communication Dinna Maningo akieleza jinsi ambavyo amekuwa akipata fursa ya kuandika habari za Uchunguzi na kupewa Tuzo katika habari hizo


Mwenyekiti wa TCCIA Bonephace Ndengo akiongea na wadau wa Habari.

Mwandishi wa Habari Azam TV Augustine Mgendi akiuliza swali juu ya usala wa waandihi wa Habari katika utendaji kazi wao.


"Ujumbe wa Katika Maadhimisho hayo Sasa ni wakati wa Habari za Uwekezaji katika Viwanda Mara"

Mejeja SIDO Mkoa wa Mara Frida Mungulu akiongelea fursa zilizopo katika Mkoa wa Mara katika Mkutano huo.

Waandishi wa Habari pamoja na Wadau wa Habari katika Mkutano huo.





Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amewahakikishia usalama waandishi wa habari Mko wa Mara na kuwataka waendelee kufuata maadili, kanuni na Misingi ya habari ili kutekeleza vyema majukumu yao.

Hayo yamebainishwa jana katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo ufanyika May tatu kila mwaka na Mkoa wa Mara imefanyika jana katika ukumbi wa Mativilla Beech Mjini Musoma na Mageni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Aidha Mkuu wa mkoa aliongeza kuwa Wandishi wa habari mkoani mara wanapaswa sasa kuzitangaza fursa zilizpo mkoani mara 

Frida Mungulu ambae ni meneja wa Sido Mara amewataka wandishi wa habari kuzitangaza fursa hizo ilikuweza kuyafikia malengo na kuunga serikali katika uchumiwa viwanda.

Amesema bado kuna haja ya watumishi mbalimbali wa serikali kwa kushirikiana na wandishi wa habari ili kuibua viwanda vidogo na kuvitangaza  ambavyo havifahamiki hivyo  kutumia taaluma yao wandishi wanaweza kutangaza na hata kuboresha.

 Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt Vicent Naahano amesema kuwa kwa kutumia viwanda mpaka sasa ndio maana walizuia kuwepo na uvuvi haramu ili kuendeleza viwanda vilivyopo Mkoa wa Mara.

Aidha Mwenyekiti wa Klabu ya  waandishi wa Habari Mkoa wa Mara MRPC Jacob Mugini amesisitiza waandishi kufuata Maadili ya Habari ikiwa ni pamoja na kutumia vyema fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Mara.





Mmiliki wa Blog ya CLEO24NEWS Frankius Cleophace akiwa katika Mkutano huo.

Wa kwanza  kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Wanduishi wa Habari Mkoa wa Mara Mugin Jacob Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini  Vicent Naahano katika Mkutano huo

Mwenyekiti MRPC Jacob Mugini akiongea na wadau wa habari ambapo amewataka waandishi wa habari kufuata misingi na kanuni za uandishi wa habari.

Meneja Ufanisi wa Mgodi na Mahusiano ya Jamii Acacia North Mara Saimon Sanga akiongea na wadau wa habari na Waandishi wa habari katika maadhimisho hayo ya uhuru wa Vyombo vya habari Mkoa wa Mara

 


Picha ya pamoja wajumbe wa kamati tenndaji MRPC Mkoa wa Mara.



Picha ya pamoja waandishi wa Habari Mkoa wa Mara.



Picha ya pamoja wadau wa Habari wakiwemo Viongozi mbalimbali.

HABARI ZOTE NA CLEO24NEWS,

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger