TRA

TRA

Wednesday, May 17, 2017

Syria yakanusha madai ya kujenga tanuri la kuteketeza waasi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 


Serikali ya Syria yasema madai ya Marekani ni kama filamu mpya ya Hollywood isiyokuwa na ukweli wowote wa uhalisia wa mambo
Serikali ya Syria imekanusha madai yaliyotolewa na Marekani kuwa imejenga eneo la kuteketeza maiti katika mojawapo ya magereza yake, na inaweza kutumiwa kuteketeza miili ya wafungwa watakaouawa. Kauli hiyo inajiri wakati duru ya sita ya mazungumzo ya amani ya Syria ikifanyika mjini Geneva Uswisi.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Syria na ambayo imetangazwa na shirika la habari la serikali ya Syria SANA imesema madai ya Marekani kuwa Syria imejenga tanuri la kuteketeza maiti katika gereza la kijeshi la Sednaya karibu na Damascus, ni kama filamu mpya ya Hollywood isiyokuwa na ukweli wowote wa hali ilivyo.
Maelfu wadaiwa kunyongwa
Hapo jana, kaimu naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa masuala ya mashariki Stuart Jones, alisema kuwa maafisa wa Marekani wanaamini kuwa tanuri hilo linaweza kutumiwa kuteketeza miili ya wafungwa katika gereza na kwamba wanaamini serikali ya rais Bashar al-Assad imeruhusu maelfu ya wafungwa ambao wamekamatwa katika kipindi cha miaka sita ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kunyongwa.
Picha ya satelaiti ya sehemu ya gereza la Sadnaya
Jones alionesha picha za satelaiti alizosema ni ya tanuri hilo. "Tunaamini kujengwa kwa tanuri ya kuteketeza maiti ni juhudi za kutaka kuficha ushahidi wa ukubwa wa mauaji ambayo yanayofanyika katika gereza la Sadnaya" Amesema Jones.
Mnamo mwezi Februari, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International liliripoti kuwa kati ya watu 20 na 50 walinyongwa kila wiki katika gereza hilo la kijeshi la Sednaya, na kwamba kati ya watu 5,000 na 13,000 walinyongwa kati ya mwaka 2011 na 2015 na huenda unyongaji huo unaendelea na kuuita uhalifu wa kivita. Madai ambayo serikali ya Syria pia iliyakanusha.
Mazungumzo Geneva
Staffan de Mistura Staffan de Mistura
Kando na hayo, waasi ya Syria na maafisa wa serikali wanakutana kandokando na mjumbe wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva katika juhudi za kusaka amani nchini humo. Hii ni duru ya sita ya mazungumzo hayo yanayoongozwa na mjumbe wa Umoja wa mataifa Staffan de Mistura. Mapema leo Staffan de Mistura na mjumbe wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar Jaafari walifanya mkutano mfupi. Wawakilishi wa upinzani walitarajiwa kukutana baadaye na de Mistura.
Mazungumzo hayo yanajiri siku kumi tu baada ya mkutano tofauti wa Kazakhstan ulioongozwa na Urusi, Uturuki na Iran kusaini mkataba uliotenga maeneo manne salama kwa raia ambako hakuruhusiwi shughuli zozoteza kijeshi. Hata hivyo mazungumzo hayo yamegubikwa na madai ya Marekani dhidi ya Syria kuhusu kujengwa kwa tanuri hilo la kuteketeza maiti.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger