Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga jana alifungua hafla ya maadhimisho ya 69ya uhuru wa
Taifa la Israeli yaliyo fanyika mjini Dodoma katika Hoteli ya Morena.
Hafla
hiyo ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Taifa hilo na uhusiono mzuri wa
kidiplomasia baina ya Tanzania na Israeli yaliratibiwa na Ubalozi wa
Israel wenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya.
Waziri
Mahiga akizungumza katika hafla hiyo aliupongeza Ubalozi wa Israel kwa
uamuzi wake wa kufanyia hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wao, Makao
Mkuu ya Serikali mjini Dodoma. Waziri Mahiga aliongeza kusema Mataifa
haya mawili Tanzania na Israel yana mahusiano mazuri ya kidiplomasia,
ikidhihirishwa wazi na idadi kubwa ya raia wa nchi hizi mbili
kutembeleana na kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano
ikiwemo utalii.
Aidha
Mahiga aliipongeza Serikali ya Israel kwa hatua kubwa ya maendeleo
waliyofikia katika maeneo mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na
kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Balozi
wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan mwenye makazi yake Jijini Nairobi,
Kenya akitoa hotuba yake alisema Ubalozi wa Israeli umechukua maamuzi ya
kufanyia hafla hiyo Mjini Dodoma ikiwa nikuunga mkono maamuzi ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma.
Aliongeza kusema kuwa hafla hiyo ni ishara ya Israel kuanziasha Ubalozi
wake nchini Tanzania.
Balozi
Vilan ameihakikishia serikali ya Tanzania kuwa Israel itaendelea kuwa
mshirika mzuri wa maendeleo ya Taifa katika maeneo ya kilimo, afya,
elimu, sayansi na teknolojia na usalama.
Israeli ilifungua kituo cha kushughulikia masuala ya viza nchini Tanzania tarehe 3 Novemba, 2016.
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye
hafla ya maadhimisho ya miaka 69 ya uhuru wa Taifa la Israel
iliyofanyika kwenye Hoteli Morena Mjini Dodoma |
|
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa unakipigwa kweye maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel |
|
Balozi
wa Israeli nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Yahel Vilan
akizunguza kwenye hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel
iliyofanyika mjini Dodoma |
|
Mhe. Balozi Vilan akisisitiza jambo |
|
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akihutubia hadhira iliyo shiriki hafla hiyo |
|
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Ramadhani (Mwinyi kulia) akifuatilia jambo, kulia ni Balozi wa
Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima |
|
Picha ya pamoja |
No comments:
Post a Comment