Wakati
uhalifu wa mtandao ukionekana kushika kasi duniani, jamii imetakiwa
kuzitumia simu za mkononi katika kulisaidia Jeshi la Polisi kubainisha
watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kama sehemu ya kutekeleza
haki yao ya kikatiba
Wito
huo ulitolewa na Mkaguzi wa Polisi, Merkiad Makumba jana kwa niaba ya
Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Korogwe , wakati akizindua duka la Kisasa
la kampuni ya simu za mkononi la Airtel katika wilaya hiyo mkoani
Tanga. Hatua hiyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya namna hiyo
ambavyo vinahatarisha ustawi wa raia na mali zao…alisema Mkaguzi
Makumba.
“
Wahalifu wengi wanatumia mawasiliano ya simu za mkononi na wamekuwa
wakiwasiliana nanyi,iwapo mtazitumia simu kwa nia njema Tanzania itakuwa
sehemu salama ya kuishi” alisema Mkaguzi Mkumba. Meneja mauzo wa Airtel
Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata
huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata
huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya
karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.
Kiango
aliongeza kwa kusema duka hili litatoa huduma nyingi pamoja na kusajili
line, kutoa huduma za kifedha za Airtel Money, kuunganisha wateja na
huduma za intaneti na nyingine nyingi , aidha alitumia fursa hilo
kuwakaribisha wakazi wa Korogwe kulitembelea duka hilo.
Mpaka
sasa Airtel imeshazindua maduka mengine kama hili katika mikoa ya
Shinyanga, Dodoma, Arusha , Manyara , Dar na Morogoro. Mpango huo wa
kuzindua maduka ya kutoa hudma kwa wateja unalenga kupanua na kusogeza
huduma za AIRTEL karibu na jamii hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma
hizi muhimu na kutatua changamoto za wateja kwa urahisi na haraka
zaidi. Mpaka ifikapo mwisho wa mwaka Airtel itazindua zaidi ya maduka
2000 nchini
Mkaguzi
wa Polisi wa Wilaya ya Korogwe, Merkiad Makumba akikata utepe wakati wa
kuzindua duka la Airtel katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Anayeshuhudia ni Ofisa wa Wateja wa Airtel Korogwe, Elen na Meneja
mauzo wa Airtel Tanga, Habibu Kiango.
SHARE
No comments:
Post a Comment