
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa (Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu
Mstaafu Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea katika
makazi yao yaliyopo Zuzu Nnje Kidogo ya Mjini Dodoma June 17, 2017
kuhudhuria Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Mzee Exavery Pinda Baba
Mzazi wa Mizengo Pinda, Pamoja nakuongoza Uchangiaji wa Ujenzi wa
Nyumba ya Paroko na Ukarabati wa Kanisa la Parokia ya ZUZU(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa kwaniaba ya familia yake akimkabidhi Mchango
wa Shilingi Milioni Kumi Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda . Kwa
ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja nakufanyia
Ukarabati wa Kanisa Parokia ya ZUZU Dodoma, Kushoto ni Msaidizi wa
Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika
June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo
ZUZU Nnje kidogo ya Mjini Dodoma

Waziri
Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa Shilingi
Milioni Kumi Mchango alizo kabidhiwa na Wziri Mkuu Kassimu Majaliwa
kwa niaba ya Familia yake , Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba
ya Paroko pamoja nakufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zinje
(ZUZU)Dodoma, Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba
Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi
ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU Nnje kidogo ya mjini
Dodoma
………………………………………………………………..
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema wazazi wana jukumu la kulea watoto kwenye
misingi ya kumcha Mungu ili Taifa liweze kuwa na watu waadilifu na
wachapakazi.
“Taifa
la watu waadilifu na wachapakazi huanzia katika ngazi ya familia. Kama
kaya zetu haziishi kwa uadilifu, ni vigumu sana kuwa na Taifa lenye
wananchi waadilifu. Ni muhimu basi familia zetu zihakikishe kuwa
tunakuwa na watoto wenye hofu ya Mungu na wenye kumcha Mungu,” alisema.
Alitoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Juni 17, 2017) wakati akizungumza na wageni
waliohudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa na nyumba ya Paroko
katika Parokia Teule ya Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Harambee
hiyo ilitanguliwa na ibada ya misa ya shukrani kwa ajili ya marehemu
Mzee Xavery Mizengo Pinda, ambaye ni baba yake, Waziri Mkuu mstaafu,
Mizengo Peter Pinda. Mzee Xavery Pinda alifariki Novemba 27, mwaka jana
katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na kuzikwa kijijini kwake Kibaoni,
wilayani Mlele, Katavi.
Waziri
Mkuu alisema wazazi wanapaswa kujitathmini juu ya malezi ya watoto wao
na kujihoji kama wamepata malezi yanayostahili. “Kupitia funzo
tulilolipata leo, tujitathmini kuhusu makuzi ya watoto wetu. Je watoto
wetu wanapata malezi stahiki? Je tunawalea katika misingi ya kutoa kwa
ajili ya Mungu au tunawafundisha wajilimbikizie mali? Je, tunawahoji
watoto wetu kuhusu utajiri wanaoupata ghafla? Au tunawapongeza na
kufurahia bila kujua wanapata wapi utajiri huo?,” alihoji.
“Nitumie
nafasi hii kuwasihi wazazi wote kwamba tujitahidi kuwekeza katika
malezi ya watoto wetu. Ili tuwe kioo cha aina ya Taifa tunalotaka
kulijenga, hatuna budi kuwalea watoto wetu katika misingi ya imani,
uadilifu na uzalendo mkubwa kwa nchi yetu,” alisisitiza.
Katika
harambee hiyo, Waziri Mkuu na mke wake walichangia sh. milioni 10
ambapo jumla ya sh. milioni 160 zilikusanywa. Kati ya hizo, sh.
111,150,000 zilikuwa ni ahadi, sh. 38,447,000 zilikuwa ni fedha taslimu
na sh. 10,403,000 zilikuwa ni vifaa vya ujenzi.
Mapema, akiongoza
ibada ya shukrani, Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma,
Padre Chesco Msaga alisema kila mtu anapaswa kumshukuru Mungu kwani
hakuna mwanadamu anayeweza kudai kuwa yuko jinsi alivyo kwa sababu ya
akili zake.
“Hata
sisi tunasahau kumshukuru Mungu hasa pale mambo yetu yanapotunyookea.
Tunadhani ni kwa akili zetu ndiyo mambo yetu yananyooka. Tunapaswa
tukumbuke kuwa maishayetu yapo mikononi mwa Mungu, na yeye ndiye anajua
njia zetu,” alisema akirejea mfano wa wakoma 10 walioponywa na Bwana
Yesu na mmoja tu ndiye alirudi kushukuru.
Kwa
upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda alisema harambee hiyo
inafuatia uamuzi wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Beatus
Kinyaiya wa kuiteua Zuzu iwe parokia.
“Sasa
hivi tulikuwa na kigango. Kuteuliwa kuwa parokia maana yake tutakuwa na
padre anakaa hapa Zuzu saa 24 na tutakuwa na ibada kila Jumapili, na
katikati ya wiki kadri ratiba zitakavyoruhusu.
“Kikubwa
tunachopaswa kufanya kufuatia uamuzi huo, ni kuhakikisha kuwa mapadre
wana nyumba ya kuishi. Sasa hivi, wa kwetu anakaa Dodoma mjini. Kwa hiyo
tuna kazi ya kukarabati kanisa, lakini kwanza tukamilishe ujenzi wa
nyumba ya mapadri,” alisema wakati akielezea madhumuni ya harambee
hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment