Na Eleuteri Mangi
Mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za
Afrika wametembelea chanzo cha maji cha Ruvu Chini uliopo Bagamoyo Mkoani Pwani
kwa lengo la kujionea namna Tanzania ilivyojizatiti katika kuhakikisha wananchi
wanapata maji ya uhakika wakati wote.
Akizungumzia ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack
Kamwewe amesma kuwa mradi wa Ruvu Chini unahudumia baadhi ya wakazi wa
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.
Mhandisi Kamwewe aliwaambia Mwaziri hao kuwa chanzo hicho cha maji kinauwezo
wa kuzalisha maji yapatayo lita milioni 275 kwa siku ambapo jiji la Dar es salaam
peke yake wakazi wake wapatao zaidi ya milioni tano wanatumia maji kiasi cha lita
milioni 450 kwa siku.
Kiasi kingine cha maji mengine ambayo yanatumika jijini dare s salaam Mhandisi
Kamwewe alisema kuwa yanazalishwa katika chanzo cha maji cha Ruvu Juu ambapo
zinazalishwa lita milioni 186 kwa siku.
Mhandisi Kamwewe aliongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanapata maji ya
uhakika kwa wakazi wa mikoa ya Pawani na Dar es salaam kwa manufaa ya maendeleo
yao na kwa ujmla taifa.
Aidha, Serikali inaendelea kuhakikisha miundombinu ya maji inakuwa imara na bora
wakati wote ambapo kwa sasa uboreshaji wa mabomba unafanyika mara kwa mara
ambapo mabomba ya zamani yanaendelea kubadilishwa na kuimarishwa matanki ya
maji yaliyopo eneo la chuo kikuu cha Ardhi, Kimara na Kibamba.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mawaziri wa Maji waliotembelea mradi huo wa Ruvu
Chini Mhe. Anna Shiweda kutoka nchini Namibia amesema kuwa wamefurahishwa na
Tanzania jinsi ilivyojipanga kuwahakikishia wananchi wake wanapata maji kwa
maendeleo yao na wame wamevutiwa kwa jinsi chanzo hicho cha maji kilivyo na vifaa
vya kisasa.
Akizunguzia upatikanaji wa maji katika nchi yake, Mhe. Anna amesema kuwa nchi yao
ni miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo eneo kubwa
linakabiliwa na ukame ambapo wakazi wa nchi hiyo maji hupatikana kwa zaidi ya
kilometa 250.
“Mkutano wetu umekuwa wa manufaa sana, tumefurahishwa na Tanzania kwa namna
ilivyojidhatiti kuwapatia wananchi wake maji, tumejifunza na tunayachukua mawazo
haya kwa manufaa ya nchi zetu” alisema Mhe. Anna.
Mhe. Waziri Anna amesema kuwa Namibia ina changamoto ya kuwa na ukame ambao
unalikumba taifa hilo lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3, kutoka Tanzania
wamejifunza mambo muhimu kupitia mkutano huo na Namibia imejipanga kutumia
teknolojia inayotumia Tanzania ili nao waweze kuwahudumia raia wake waweze
kupata maji safi na salama.
Maonesho ya wiki ya maji yanayofanyika Dar es salaam yanahudhuriwa na Mawaziri wa
Maji kutoka nchi 38 zikiwemo Tanzania ambayo ni mwenyeji wa maonesho hayo,
Sudan, Kongo, Lesotho,Madagaska, Burundi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Senegal,
Togo, Liberia, DRC na Zimbabwe.
Nchi nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Libya, Kenya, Misri, Ivory Coast, Cameroon,
Msumbiji, Zambia, Sudan Kusini, Bukina Fasso, Afrika Kusini, Mali, Ethiopia, Benin,
Mauritania, Uganda na Djibouti.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa
akiwaelezea baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika waliotembelea
mtambo huo kujifunza namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia maji
wananchi wake.
Baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika
wakitembelea maeneo mbalimbali ya mtambo Ruvu Chini kujifunza
namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia maji wananchi wake.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwewe
akiwaeleza baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika namna mradi wa
Ruvu Chini unavyowahudumia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.
Mhifadhi wa Mji Mkongwe wa Bagamoyo Noel Laswai akiwaeleza
baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika namna mji wa kale wa
Kaole ulivyokuwa tangu karne ya 13.
Mhifadhi wa Mji Mkongwe wa Bagamoyo Noel Laswai akiwaeleza
baadhi ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika mti aina ya mpingo
unaohifadhiwa katika eneo la Kaole namna unavyotumiwa ambao mti huo
una zaidi ya miaka 30.
Waziri wa Mji wa Namibia Anna Shiweda na Waziri wa kutoka nchini Libya
Assayed Abdurrahaman Naji wakiangalia baadhi ya mabaki ya viumbe vinavyoishi
baharini katika ufukwe wa Bagamoyo wakati wa ziara ya kujifunza namna Tanzania
inavyotunza rasilimali zake kwa mnaufaa ya sasa na baadaye.
madhari za baadhi ya maeneo ya fukwe za wilaya ya Bagamoyo zinavyovutia kwa
utalii na michezo mbalimbali.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
SHARE
No comments:
Post a Comment