Meneja Pep
Guardiola amesema Benjamin Mendy atasubiri kwa wiki mbili ama tatu baada
ya Manchester City kuicharaza Real Madrid 4-1 mechi ya kirafiki mjini
Los Angeles.
Mashabiki takriban 93,000 waliisaidia City kushinda mechi yao ya kwanza ya maandalizi ya msimu ujao kupitia mabao yaliofungwa na Nicolas Otamendi, Raheem Sterling, John Stones na Brahim Diaz.
Kutokuwepo kwa Mendy, Danilo alianzishwa katika uwanja wa Los Angeles huku beki huyo wa kushoto akianzishwa dhidi ya timu yake ya zamani baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 26.5.
''Leo tumeona vile tunavyocheza vizuri'',Guardiola alisema.
''Ni mshindani. Yeye na Kyle walisaidia kutengeneza kiungo chetu cha ulinzi .Waliwasiliana .Tuna furaha sana kuhusu hilo''.
SHARE
No comments:
Post a Comment