Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ Mkoa wa
Mara Julai 27, 2017 imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya Musoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma
(MUWASA) Hawaiju Said Gantala kwa makosa 15. Gantala amefikishwa mbele ya Hakimu Karimu Mushi na Mwendesha
mashitaka wa TAKUKURU, Moses Malewo akikabiliwa na mashtaka ya kughushi,
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za
kupotosha katika Benki za CRDB na NBC matawi ya Musoma.
No comments:
Post a Comment