Msanii wa Bongo flava na mfalme wa
miduara AT, akiongelea utamaduni wa kiswahili na raha za pwani kwenye
jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza
utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae kuonesha onesho kali ya
nyimbo zake zilizotamba na zinazoendelea kutamba kwenye anga ya bongo na
kimataifa. Kongamano hilo linaloambatana na tamasha la Mswahili na
lugha yake huandaliwa na Swahili Media Network na hufanyika mara moja
kila mwezi. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT akichengua mashabiki wake kwa wimbo mmoja wapo wa mduara.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT usipime ni balaa
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa
buradani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku
ya Jumamosi July 22, 2017 Hampton Inn, College Park, Maryland.
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye jopo la kongamano la raha za Pwani
Aisha akifungua pazia kwenye jopo la
kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni
wa Mswahili na lugha yake.na baadae kumkaribisha mratibu wake
Mgaza (hayupo pichani).
Mratibu wa Raha za Pwani Bwn. Mgaza
akiuelezea Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano
la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi Julai 22, 2017 College
Park, Maryland.
Bi Rukia akichangia nini maana ya
Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za
pwani lililofanyika siku ya Jumamosi Julai 22, 2017 College Park,
Maryland na huku akitoa rai kwa wazazi ughaibuni kuacha kudharau
utamaduni wa wetu na wafanye kazi ya ziada kuwafundisha watoto wa
ughaibuni lugha ya Kiswahili na utamaduni wake.
Mama mitindo na mkurugenzi wa Miss
Tanzania USA MaWiny Casey akichangia vazi la khanga na utamaduni wa
Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani
lililofanyika siku ya Jumamosi Julai 22, 2017 College Park, Maryland.
Mama mitindo na mkurugenzi wa Miss
Tanzania USA MaWiny Casey akimkabidhi tuzo Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza
linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) -
Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA, aliefuatana na Msanii maarufu wa nyimbo
na ngoma ya Muduara- Bwana ALI RAMADHAN ALI, al-maarufu kwa jina la MR.
AT kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya
Jumamosi Julai 22, 2017 College Park, Maryland.
Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza
linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) -
Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA akiongelea muziki unavyodumisha utamaduni
wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani
lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Watoto Imani (kushoto)naAaliyah
wakicheza moja ya mchezo ya watoto wanavyocheza kwa Kiswahili kama moja
ya kudumisha Kiswahili na utamaduni wake.
--
SHARE
No comments:
Post a Comment